HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Saturday, 21 May 2016

Jarida maarufu la Marekani The Source lampa shavu Alikiba

image 

Jarida la The Source limeipa kipaumbele habari ya Alikiba kusaini deal la kimataifa na label kongwe ya Sony Music ambapo limedai ni msanii wa pili kusaini deal ya ukubwa huo kwa Afrika baada ya Davido.
image
Hiyo inathibitisha ama kutoa hofu ya mashabiki wa muziki kuwa deal hiyo haina tofauti na zile zilizofeli za wasanii kama Keko na Rose Mhando ambao wao mkataba ulikuwa ni kwa Afrika pekee.
Kwa mujibu wa meneja wa Alikiba, Seven Mosha, Sony Music itawekeza nguvu, fedha, nyenzo na utaalam kuhakikisha Alikiba anakuwa msanii wa kimataifa.
Hiyo inamaanisha itagharamia kila sumuni itakayotumika kurekodi muziki ikiwemo kutumia waandishi wa muziki mahiri duniani, kulipia video zake, kumuunganisha na vyombo vya habari vya kimataifa, kusimamia utengenezaji wa album na kuisambaza duniani kote na vingine.
Kwa sasa Kiba hatotumia tena hela yake kufanya muziki.
Pia Sony watahusika katika kumkuza zaidi Alikiba kimuziki pamoja na kufanya utafiti wa kina kumtengenezea njia ya mafanikio.
Deal la Alikiba na Sony Music limepokelewa kwa furaha kubwa na wapenzi wa muziki nchini.

No comments:

Post a Comment