HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Wednesday, 22 June 2016

Nuh Mziwanda achora tattoo mpya ya jina la mpenzi wake wa sasa aitwae ‘Nawal’



Mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda amechora tattoo mpya katika mkono wake wa kushoto ya jina la mpenzi wake wa sasa aitwae ‘Nawal’.
Nuh akiwa na mpenzi wake mpya aitwae Nawal
Nuh akiwa na mpenzi wake mpya aitwae Nawal
Mwimbaji huyo ambaye bado ana tattoo nyingine mkononi ya mpenzi wake wa zamani Shilole, amekiambia kipindi cha Clouds E kinachoruka katika runinga ya Clouds TV kuwa, haoni kama ni tatizo kuchora tattoo ya mpenzi wake huyo.
“Yeah nimechora (huku akiionyesha) nimempenda na yeye ananipenda,” alisema Nuh. “Huyu ana mapenzi ya dhati kwangu, Shilole alikuwa hataki niwe na washkaji, yaani nikae ndani tu hata mwaka mzima, lakini kwa mpenzi wangu huyu yupo poa sana, anawapenda marafiki zangu, anawapikia geto tunakula, kwa hiyo kwangu mimi tattoo ni kama ndoa,”
kk
Nuh na Mpenzi wake
Kwa upande wa mpenzi wake huyo aitwae, ‘Nawal’ alisema anafurahi kuwa na Nuh.
“Ananipenda na mimi nampenda, sioni tatizo kuchora tattoo kwa ajili yangu,” alisema Nawal

No comments:

Post a Comment