HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Thursday, 30 June 2016

Ongezeko la asilimia 18 (VAT) ya makato ya miamala ya benki kuanza Ijumaa hii (July 1)



Ijumaa hii itakuwa tofauti kwa wateja wengi wa benki nchini. Ni kwasababu benki karibu zote kuanzia July 1, zitaanza kutumia sheria mpya ya fedha ya mwaka huu iliyopitishwa na bunge la 2016/17.
6d0d9cc2-bf19-49e7-b776-984e106bd1aa
Kupitia tangazo lake kwa wateja, benki ya CRDB imedai kuwa ongezeko la asilimia 18 zitatozwa katika gharama za huduma ya benki kuanzia Ijumaa hii, July 1.
“Ongezeko hili (VAT) litakatwa kutoka katika akaunti akaunti ya na kama muamala hautapita kwenye akaunti, mteja atalipia kwa fedha taslimu, Kulingana na sheria hii, hakutakuwa na makato ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) katika riba,” imesema taarifa hiyo.
Benki ya NMB nayo imetoa taarifa hiyo kwa wateja wake.
33c0cb6b-e2cb-4ecb-b825-fc75c8a1783a
Tafsiri ya ongezeko hilo kutoka kwa mfanyakazi wa benki moja niliyemuuliza ni kuwa kama benki ilikuwa ikikata shilingi 1,000 kwa muamala unaoanzia shilingi elfu 10, kwa sasa mteja atakatwa shilingi 1,800 ambazo ni sawa na asimilia 18.

No comments:

Post a Comment