HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Monday, 27 June 2016

Supastaa wa Zimbabwe Jah Prayzah amfuata Diamond Dar kurekodi collabo yao

Mwanamuziki maarufu wa nchini Zimbabwe, Mukudzei Mukombe anayejulikana zaidi kwa jina la Jah Prayzah alilazimika kusafiri hadi Dar es Salaam kuja kukamilisha collabo yake na Diamond Platnumz.
image
Jah Prayzah ambaye hujulikana pia kwa jina la Musoja kutokana na kupenda kuvaa nguo za kijeshi, amemshirikisha Diamond kwenye wimbo wake uitwao Watora Mari.
image
Wimbo huo utapatikana kwenye album yake mpya na ya saba, iitwayo Mudhara Vachauya itakayozinduliwa August 12 kwenye ukumb wa kimataifa wa mikutano wa Harare (Harare International
Conference Centre).
image
Akiongea na gazeti la The Zimbabwe Standard, Jah Prayzah alisema ameamua kumshirikisha Diamond kutokana na umaarufu wake barani Afrika.
image
“Ni nzuri kushirikiana na watu maarufu kama hao barani kwasababu watu wengi zaidi watakufahamu kupitia yeye na ni suala la kusaidiana ili kwenda mbali zaidi,” alisema.
Wimbo huo ulirekodiwa kwenye studio za Wasafi jijini Dar es Salaam na staa huyo hakusita kuelezea furaha yake kwenye Instagram.
image
“Surely dreams come true no matter how long it might take,happy to say that we did a collabo with one of Africa’s finest musicians @diamondplatnumz,” aliandika Ijumaa hii.
“It could not be more better than this,we produce good music for a living!!!!!Cant wait for August 12 #ALBUM LAUNCH #HICC.”
image

No comments:

Post a Comment