HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Thursday, 23 June 2016

Video: Davido na Trey Songz wakutana tena Marekani, collabo yao yakamilika


Msanii wa Nigeria, Davido amepost kipande cha video kinachomuonyesha akiwa kwenye klabu moja ya usiku huko Atlanta akiwa na staa wa Marekani, Trey Songz wakiashiria ule wimbo wao walioahidi kuwa upo tayari.
trey-n-dav
Kwa mara ya kwanza Davido alionana na Trey Songz nchini Nigeria, Disemba mwaka jana staa huyo alipotembelea nchi hiyo kwa ajili ya kufanya show kwenye tamasha la Rhythm Unplugged, lakini kwa sasa wameonekana kukamilisha ahadi ya wimbo wao walioahidi kufanya collabo mbele ya mashabiki wa Nigeria.
Inadaiwa kuwa jina la wimbo huo ni ‘Won Le Ba’ na umeandaliwa na mtayarishaji wa muziki, Shizzi. Davido amekuwa kimya bila ya kutoa wimbo wowote tangu aliposaini dili na kampuni ya Sony Music, Januari 21 mwaka huu.
Tazama video hapa.

No comments:

Post a Comment