Hii
imeripotiwa na BBC swahili kuwa magari yanayotumia nguvu za umeme
yameanza kuuzwa Afrika Mashariki kwenye nchi ya Kenya kwa mara ya
kwanza. Magari hayo hayatumii mafuta hata kidogo hii ikiwa na maana
kwamba hayatoi moshi au gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani kwa
hivyo yanafaa mazingira.
Msimamizi wa kampuni Knights Energy inayohamasisha watu watumie magari ya aina hiyo, Francis Romano amesema…..>>>”Watu wengi wamekuwa wakiduwazwa na gari hili mitaani hapa jijini Nairobi na wengi wamependezwa nalo’
Bei ya gari hilo aina ya Nissan Leaf ni dola za kimarekani 10,000 ambazo ni kama Tsh milioni 21.88
Katika
taarifa hii ya BBC swahili imeainisha baadhi ya faida za matumizi ya
gari hilo kuwa ni pamoja na mwenye gari kutoathiriwa na kupanda na
kushuka kwa bei ya mafuta pia linaendeshwa kwa njia karibu sawa na gari
la kawaida.
Aidha
imeelezwa kuwa gari hilo lina uwezo wa kusafiri umbali wa takriban
kilomita 90 hadi 135 kabla ya betri zake kuisha chaji, kasi yake ya juu
zaidi ikiwa kilomita 180 kwa saa.
Kuna
baadhi pia ya changamoto ambazo mtu anaweza kukutana nazo kutumia gari
hilo ambazo ni pamoja na ukosefu wa vituo vya kuchaji gari hilo na pale
ambapo mtu amekwama akiwa katika maeneo ya mashambani ambapo hamna nguvu
za umeme au pia vituo vya kuweka chaji.
Gari hilo lina chaji tatu, ya kwanza ina uwezo wa kuweka chaji kikamilifu kwa muda wa saa nane, ya pili ina uwezo wa kuweka chaji kwa takriban saa nne, huku ya tatu ikiwa na uwezo wa kuweka chaji kwa kati ya takriban dakika 15 na saa mbili.
No comments:
Post a Comment