Thursday 7 July 2016
Polisi Marekani wawaua watu weusi wawili katika matukio mawili tofauti yaliyozua hasira kali
Tukio jipya zaidi limetokea kwenye jimbo la Minnesota wakati maandamano yakiendelea kutokana na kuuawa kwa mtu mwingine mweusi huko Louisiana.
Mpenzi wa Philando Castile alirekodi tukio zima na kulirusha live kwenye Facebook na kumuonesha mtu huyo akiwa ameloa damu huku polisi akimwelekea bunduki.
Mpenzi wake anasema alipigwa risasi wakati alipotaka kuchukua leseni yake ya udereva.Castile alisimamishwa na polisi kutokana na taa ya gari yake kuwa na taa iliyovunjika kwa mujibu wa mpenzi wake anayejulikana kwa jina Lavish Reynolds.
Kabla ya kupigwa risasi, alimweleza polisi huyo kuwa alikuwa ameruhusiwa kutembea na bunduki na alikuwa nayo hapo.
“You shot four bullets into him, sir. He was just getting his license and registration, sir,” Ms Reynolds anasikika akisema kwenye video hiyo.
Polisi wamesema uchunguzi unaendelea na ofisa huyo amepumzishwa.
Tukio hilo limekuja baada ya kuuawa kwa Alton Sterling, aliyepigwa risasi na polisi kwenye tukio lililotokea huko Baton Rouge, Jumanne.
Mamia ya watu waliandamana kwa siku mbili kufuatia mauaji hayo.
Video imesambaa Jumatano hii Sterling akiwa amelazwa chini na polisi na baada ya kupigwa risasi za kifuani takriban sita.
Polisi wanadai kuwa Mr Sterling alikuwa na silaha.
Tukio hilo lilitokea nje ya duka hata hivyo mmiliki, Abdullah Muflahi, alisema kuwa mtu huyo hakuwa tishio kwa maofisa hao wakati akipigwa risasi.
Sterling, baba wa watoto watano alifariki masaa kadhaa baadaye.
Maofisa waliohusika wamebainika kuwa ni Blane Salamoni na Howie Lake II, nao wamepumzishwa kwa muda.
Matukio hayo yamesababisha hasira kubwa kwa watu mbalimbali wakiwemo mastaa. The Game, Drake, Tyrese, Chris Brown na wengine wameyalaani vikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment