HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Friday, 1 July 2016

Ureno mdogo mdogo yatinga nusu fainali ya Euro 2016



Timu ya taifa ya Ureno imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Euro inayoendelea huko nchini Ufaransa baada ya kuifunga timu ya taifa ya Poland kwa mikwaju ya penati 5-3.
gareth-bale-23324
Mpaka dakika 90 zinamalizika timu hizo zilifanikiwa kufungana bao 1-1 na hivyo ziliongezwa dakika 30 ili kutimiza dakika 120 lakini hata hivyo hawakuweza kufungana.
Poland ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli kwenye dakika ya 2 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake hatari, Robert Lewandowski nao Ureno walisawazisha goli hilo kupitia kwa mchezaji wake kinda, Renato Sanchez kwenye dakika ya 33.
Ricardo Quaresma alikuwa shujaa kwa timu yake baada ya kupiga penalti ya mwisho iliyoivusha katika hatua nyingine huku kiungo wa Jakub Blaszczykowski akikosa mkwaju wa penalti kwa upande wa Poland.
Ureno itakutana katika hatua ya nusu fainali na mshindi wa mchezo kati ya Wales na Ubelgiji.

No comments:

Post a Comment