HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Wednesday 6 July 2016

VIDEO: Polisi waelezea chanzo cha ajali ya mabasi ya City Boys Singida


July 04 2016 maeneo ya Maweni-Kintiku Singida mabasi mawili ya kampuni ya City Boys yaligongana na kusababisha vifo vya watu 30 na majeruhi 54 ambapo hadi leo wamebaki majeruhi 33 wakiendelea na matibabu. Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi, kikosi cha usalama barabarani, Mohamed Mpinga amesema
>>>’kwa ajali iliyotokea Maweni Singida siyo ajali ya kawaida bali ni tukio la kufanya mauaji bila kukusudia, hivyo polisi imedhamiria kuwafikisha mahakamani madereva waliohusika na ajali hiyo kwa mashtaka ya mauaji bila kukusudia kutokana na taarifa za awali za chanzo cha kutokea kwa ajali hiyo ni kwamba madereva wa mabasi hayo walikuwa wakifanya mzaha wakati wa kupishana.
>>>Aidha tumewasiliana na wenzetu wa SUMATRA, kampuni ya mabasi ya City Boys na makampuni mengine yaliyohusika katika ajali yafungiwe kutoa huduma za usafirishaji katika njia zote hapa nchini.

No comments:

Post a Comment