Dully Sykes ambaye wimbo wake huo ulifanyika kwenye studio za wasafi na gharama zote za video kugharamiwa na lebo hiyo amesema yeye yuko kwenye studio hizo kama kaka tu,na walichofanya WCB ni kama kulipa fadhila kwa kaka yao.
“WCB, mimi ni nyumbani,sijasaini mkataba na wala hatuna hizo plan,mimi nipo hapa kama kaka.Na mimi ndio mtu wa kwanza kumkimbiza Diamond kufungua studio kwa hiyo nafurahi alifanya hivyo pia napenda producer wa hapa,ndio wa maana nimeamua kufanya kazi hapa na wao wamegharamia kila kitu kama kulipa fadhila” alifunguka Dully Sykes.
No comments:
Post a Comment