Good news ni kwamba Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na kampuni ya Makini Road Safety Foundatini imeturahisishia njia nyepesi ya kukabiliana na ajali za barabarani ambapo kwa kutumia application ya MakiniApp ambayo ukiwa nayo katika simu yako inakusaidia kujua mwendokasi wa dereva kwenye gari ulilopanda.
Nakukutanisha msemaji mkuu wa MakiniApp Irene Kidunda…>>> ‘MakiniApp
hii ni application ambayo inamuwezesha mtumiaji kufahamu kiwango halisi
cha mwendokasi wakati anaoutumia dereva wakati wa safari kupitia simu
yake‘
‘Ikiwa dereva
anatembea kwa mwendokasi usiotakiwa mtumiaji anaweza kuchukua hiyo
taarifa na kuituma katika kikosi cha usalama barabarani kupitia hiyohiyo
simu yake ili askari wamchukulie hatua dereva huyo‘ –Irene Kidunda
‘Uzuri
wa kuwa na application hii ni kwamba hatakama hutakuwa na mtandao kwa
muda huo bado utakuwa na uwezo wa kurekodi mwendokasi wote na kisha
ukampatia askari polisi utakayemkuta barabarani na bado ikawa na msaada‘ –Irene Kidunda
Kamanda wa Polisi kikosi cha usalama barabarani Mohamed Minga anasemaje kuhusu hatua hii?…>>>’Tumekuwa
tukitoa namba ya simu ambayo abiria wataitumia kutoa taarifa za usalama
barabarani ambazo ni 0682887722 na ukituma taarifa hizo sisi
tunazifanyia kazi‘
‘Tunaamini
mfumo huu wa MakiniAppy utatusaidia sana kudhibiti mwendokasi na
kupunguza ajali za barabarani licha ya mfumo wa tochi tuliozoea kuutumia‘ –Mohamed Minga
No comments:
Post a Comment