HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Wednesday 14 September 2016

Ben Pol kuja na remix ya Moyo Mashine akiwa na ChidinmaBy Rama Nnauye

ben-pol1

Mkali wa muziki wa RnB Bongo, Ben Pol amesema anatarajia kuja na remix ya wimbo wake, 
Moyo Mashine akiwa na msanii wa Nigeria, Chidinma.
Hadi sasa ‘Moyo Mashine’ umekuwa wimbo wa Ben Pol wenye mafanikio makubwa.
chidinmaekile-20160914-0002
Chidinma
Muimbaji huyo,kuwa remix hiyo itakuwepo kwenye album yake mpya.
“Ngoma ambayo inakuja ni Moyo Mashine remix ambayo nimefanya na Chidnma kutoka Nigeria
,” amesema. “Nilimsikilizisha nyimbo nyingi lakini aliupenda huo, nikaona sawa,” ameongeza.
“Na pia kuna nyimbo nyingine tena nimefanya naye muda wake ukifika nitauzungumzia huo wimbo.
 Na hizi nyimbo zote zitakuwa katika album yangu mpya ambayo nategemea itatoka baada ya mwezi
 Disemba.”

No comments:

Post a Comment