Rihanna anapenda watoto waende shule. Taasisi yake ya Clara Lionel Foundation imeungana na Global Partnership for Education and Global Citizen katika mradi wa miaka mingi wa kusaidia elimu duniani.
Kupitia mradi huu, Rihanna ana matumaini ya kuwatetea watoto zaidi ya robo bilioni ambao hawapo shuleni pamoja na wanafunzi milioni 330 ambao hawajifunzi kitu katika shule walizopo.
Akiwa kama balozi mpya wa dunia wa GPE, Rihanna anatarajiwa kufika katika nchi zinazoendelea zaidi ya 60, akizipa kipaumbele zile zenye uhitaji zaidi zikiwemo zenye migogoro. Tanzania ni moja kati ya nchini zenye changamoto kubwa za elimu.
Mwenyekiti wa GPE, waziri mkuu wa zamani wa Australia, Julia Gillard amesema anayo furaha kubwa kuingia ushirikiano na Rihanna, ambaye jina lake halisi ni Robyn Fenty.
Rihanna alianzisha Clara Lionel Foundation mwaka 2012 kwa kumbukumbu ya bibi na babu yake, Clara na Lionel Braithwaite.
No comments:
Post a Comment