HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Monday 26 September 2016

Salamu za Mrisho Mpoto kwa Diamond Platnumz kuhusu wimbo wa Salome


Moja kati ya wasanii wenye heshma kubwa nchini na watunzi wa mashairi na nyimbo zenye mahadhi ya kiafrika, Mrisho Mpoto, kupitia mtandao wa Instagram amemsifia Diamond Platnumz kwa wimbo wake mpya wa Salome na kusema kuwa amemfurahisha sana kwani amefanya wimbo wenye asili ya kwetu Tanzania na hiyo ni heshima kwa nchi.
 >>Nassibu kiukweli nimefurahishwa sana na kazi yako ya#Salome imeonyesha ukomavu Mkubwa na team work, kikubwa ukiwa unafanya kazi zenye test ya nyumbani unatupa heshima kama nchi na inakuonyesha wewe ni nani? na nani siyo wewe? Nassibu Mwenda kwao siku zote haogopi Giza, nenda lakini waambie nna kwetu, kama ulivyofanya kwenye Salome. Sisi ni wabantu bwana tunaruhusiwa zaidi ya mmoja, na Mimi ntamtafuta Salome wangu wa ukubwani ashike magoti nisimame kama ngongoti japo nna kitambi ntainama kidogo!!@diamondplatnumz @babutale
mpoto
Video ya wimbo wa Salome inazidi kufanya vizuri kwenye mtandao wa Youtube ukiwa umetazamwa na zaidi ya watu milioni 2 chini ya wiki moj

No comments:

Post a Comment