Hatimaye mwali amewasili. Ni ndege ya kwanza ya ATCL, Bombadier Q400 NextGen.
Bombadier Q400 NextGen baada ya kuwasilia JNIA, Dar Jumanne hii
Ndege hiyo imetokea Canada ilikotengenezwa na kupokelewa kwa shangwe huku mapokezi hayo yakiongozwa na katibu mkuu wa uchukuzi, Dkt Leonard Chamriho.
Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 76.
Ndege ya pili itawasili baada ya wiki moja na Rais John Magufuli ataongoza mapokezi rasmi ya ndege hizo.
Ndege
mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada
ilikotengenezwa.
Ndege hiyo
aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na
kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya
inayotua katika nchi yake (Water Salute).
Baada ya
kupokewa ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing
Ukonga). Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu
Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa
kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili
ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa
baadaye.
No comments:
Post a Comment