HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Tuesday 24 January 2017

Joti aeleza kwanini Orijino Komedi haipo kwenye TV siku hizi

Kwako mfatiliaji wa mabingwa wa kuchekesha wanaoishikilia rekodi ya Wachekeshaji waliotazamwa sana kwenye TV Tanzania kuanzia time hiyo ya ZE Comedy mpaka Orijino Komedi walivyokua wanawafanya watu wawahi TV zao kila Alhamisi jioni.
Ni kitambo kidogo hatujawaona Orijino Komedi kwenye TV (TBC 1) na inawezekana maswali tuliyonayo ni mengi lakini hakuna hofu tena maana tumempata Joti na amekubali kuongelea kwa ufupi.
Kama kundi tunataratibu zetu na ndio maana tumejaribu kutumia muda wa mwaka mmoja kupumzika maana toka tuanze kufanya kazi hatujawahi kupumzika, tulivyopomzika pia sio kukaa kimya tukaangalia project za kila mtu binafsi na ndio maana unaona kila mtu na shughuli zake‘ – Joti
Ukimfatilia Mpoki kuna shughuli zake anafanya na inajulikana, Masanja pia vivyo hivyo… na mimi nimefungua Youtube channel yangu ya Joti TV, nafikiri mwaka huu tunaweza kurudi kazini pia‘ – Joti

No comments:

Post a Comment