HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Wednesday, 25 January 2017

Nchi 7 ambazo raia wake watazuiliwa kuingia Marekani maneno ya Trump



Taarifa za baadhi ya maafisa wa bunge la Marekani (Congress) na mtaalamu katika Idara ya Uhamiaji zimeeleza kwamba Rais Trump leo Jumatano anatarajia kusaini miswada kadhaa ikiwemo ya kusimamisha kwa muda utoaji visa kwa raia wa nchi za Kiarabu.
January 25, 2017 Trump aliandika kwenye Twitter kwamba itakuwa siku kubwa kwa usalama wa taifa, pamoja na mambo mengine tutajenga ukuta.
Ufafanuzi uliotolewa umeeleza kuwa Trump anakusudia kuzuia kwa miezi kadhaa wahamiaji kuingia Marekani isipokuwa wale aliowataja kuwa ni wa “Jamii za wachache wanaodhulumiwa” hadi zitapopitishwa sheria kali na ngumu kuhusiana na uingiaji wakimbizi nchini humo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, maombi ya vibali kwa raia wa Syria, Iraq, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen vitazuiliwa.
Vilevile katika ukurasa wake Twitter, Trump ameonesha pia msimamo wake wa kujenga ukuta kwenye mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Mexico na kusisitiza kuwa ujenzi huo utatekelezwa kwa namna yoyote.

No comments:

Post a Comment