HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Friday, 21 April 2017

Diamond kuandika historia tena

Diamond ametangaza siku ambayo ataachia manukato yake ya mapya yajulikanayo kama Chibu Perfume.

Hatua hiyo imekua ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wake wengi tangu alipoweka hadharani ujio wa biashara hiyo mwezi Novemba mwaka jana.
Kupitia mtandao wa Istagram, Hitmaker huyo wa ‘Marry You’ ametaja siku ya kuingiza sokoni kwa perfume, “The Only Scent you deserve, @chibuperfume by Diamond Platnumz coming out this friday!! #TheScentYouDeserve.”
Endapo hilo litafanikiwa Diamond ataingia kwenye orodha ya mastaa wakubwa duniani walifanikisha kuachia perfume zao kama Nicki Minaj, Beyonce, Diddy, David Beckham na wengine. Hatua hii imepokelewa kama ya kihistoria kwa wengi akiwa ni msanii wa kwanza wa kiume Tanzania kuachia bidhaa ya perfume kupitia brand yake.

No comments:

Post a Comment