Jina la staa wa soka wa kimaifa wa Ureno
Cristiano Ronaldo lilirudi kwenye headlines baada ya usiku wa April 12
2016 kuisaidia klabu yake ya Real Madrid kufuzu hatua ya nusu fainali ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuifungia hat-trick dhidi ya Wolfsburg.
Baada ya hat-trick hiyo Ronaldo ameweka
rekodi kadhaa ndani ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na nje ya Ligi hiyo,
Ronaldo ndiye mchezaji anashikilia rekodi ya kufunga magoli zaidi ya 30
katika misimu sita ya Laliga mfululizo, hat-trick ya jana imemfanya
Ronaldo kuweka rekodi ya kufunga zaidi ya goli 45 katika kila
msimu akiwa na Real Madrid.
Kama ulikuwa hujui Ronaldo anashikilia
rekodi ya kufunga jumla ya goli 17 katika msimu 2013/2014 wa Ligi ya
Mabingwa Ulaya idadi ambayo haijafikiwa na mchezaji yoyote, ila
headlines mpya ni kuwa Ronaldo anakaribia kuvunja rekodi hiyo msimu huu,
kwani hadi sasa amefunga jumla ya goli 16
No comments:
Post a Comment