HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Monday, 18 April 2016

Nilimuomba kolabo Diamond sababu anajituma sana – 2 Face

vanessa-mde-and-2faceidibia-styled-by-fawwie-559x520


Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM Jumamosi hii akiwa Nigeria, muimbaji huyo wa ‘African Queen’ alisema ni yeye ndiye aliyemuomba Diamond wafanye wimbo wa pamoja.
Amedai alikuwa akionana na Diamond kipindi alipofululiza kwenda Nigeria, na alivutiwa jinsi ambavyo anajituma kufanya kazi zake kwa nguvu.
“Unajua [Diamond] ni kijana ambaye unamuona anapanda, anafanya kazi kwa bidii, anakazana sana na anajituma kwa kweli unaona kabisa huyu anapanda, nikaongea naye ili ipite kolabo kati yetu kwahiyo tutegemee kazi nzuri,” alisema.
Kwa upande mwingine 2 Face alidai kuwa Vanessa Mdee ni miongoni mwa hazina ya wasanii wa kike Afrika wenye sifa za kutoboa Kimataifa.
“Nilikutana na Vanessa kwenye Coke Studio, well ni msanii mwenye sifa zote za kuwa msanii mkubwa duniani, tayari kakamilika kwa kila kitu,” aliongeza.

No comments:

Post a Comment