Ni asilimia 1 katika paundi milioni 1.7 zilizochangwa na mastaa na wafanyabiashara wa Uingereza kwaajili ya kuisaidia taasisi iliyoanzishwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, zimewafikia walengwwa, imebainika
Taasisi hiyo inayosaidiwa pia na Princess Beatrice na David Beckham
inachunguzwa. Wachangiaji wakiwemo Bono, Frank Lampard na Christine
Bleakley, waliambiwa kuwa fedha hizo zingetumika kujenga hospitali na
kuwapa elimu watoto maskini nchini Ivory Coast.
Lakini Mail Online imeripoti kuwa ni £14,115 tu ndizo zilizowafikia
walengwa. £439,321 zilitumika kuandaa hafla ya kifahari ya uchangiaji
iliyopambwa na burudani za muziki kutoka kwa wasanii wakubwa.
Mastaa wengine wanaoisaidia taasisi hiyo ni pamoja na Pele, John
Terry, Roger Federer na Donna Air, girlfriend wa kaka yake na Duchess of
Cambridge, James. Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich naye alidaiwa
kuchangia kiasi kikubwa cha fedha.
Pia kuna maswali kuhusu fedha za udhamini kutoka kwa makampuni kama
Pepsi, Nike ma Samsung, ambazo Drogba alidai zimeenda kwenye charity
No comments:
Post a Comment