Moto wa burudani utawaka katika jiji la Mwanza Jumamosi ya wiki
ijayo ambapo msanii maarufu wa muziki wa Bongofleva kutoka Marekani
NE-YO atakapo shusha bonge ya shoo kwa kushirikiana na wasanii wa hapa
nchini katika uwanja wa CCM Kirumba kwenye onyesho lililotayarishwa na
Jembe Media chini ya Udhamini wa Vodacom Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina
Nkurlu(Katikati)akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo,(hawapo pichani) wakati wa kutangaza baadhi ya wanamuziki nchini
ambao watatoa burudani pamoja na Mwanamuziki nguli kutoka Marekani
NE-YO, katika Uwanja wa (CCM) Kirumba jijini Mwanza kwenye tamasha la
Jembeka na Vodacom Festival 2016.Wengine katika picha kushoto ni
Mwakilishi wa NE-YO,E.Jay Mathews na Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni
Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo,Dkt.Sebastian Ndege
Akiongea juu ya onyesho hilo la kihistoria katika ukanda wa ziwa
Magharibi,Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alisema kuwa
Vodacom inayo furaha kudhamini tamasha hili kubwa litakaloleta
burudani ya muziki kwa wateja wake na wananchi kwa ujumla.
Aliwataja baadhi ya wanamuziki watakaowasha moto kumsindikiza NE-YO
kuwa ni Diamond,Ney wa Mitego,Fid Q,Ruby,Baraka the Prince,Juma
Nature,Mr.Blue,Stamina,JJ Bendi na wengineo.
Mwakilishi wa Mwanamuzi nguli toka nchini Marekani NE-YO,E.Jay
Mathews (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati wa kutangazwa kwa wasanii watakaotoa burudani pamoja na
mwanamuziki huyo katika tamasha la Jembeka na Vodacom festival 2016,
litakalofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wapili
(kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji
wa tamasha hilo,Dkt. Sebastian Ndege, Matina Nkurlu Meneja Uhusiano wa
Vodacom Tanzania, George Sozigwa Mkuu wa masuala ya ulinzi na Usalama wa
tamasha hilo
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa
tamasha hilo, Dkt.Sebastian Ndege aliwataka wapenzi wa muziki
kujitokeza kupata budurani ya mwaka katika tamasha hilo na mipango ya
tamasha hilo kubwa imekamilika na kuwataka wapenzi wa muziki wa Mkoa wa
Mwanza wakae mkao wa kula wa ya karne.
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul maarufu kama
Diamond Platnumz akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo
pichani)kuhusiana na jinsi atakavyoshiriki kutoa burudani na kuimba
wimbo wa pamoja na mwanamuzi NE-YO wa nchini Marekani katika tamasha la
Jembeka na Vodacom festival 2016,litakalofanyika katika uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza,Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe
ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo,Dkt.Sebastian Ndege,Matina Nkurlu
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania
Kuhusiana na viingilio alisema kuwa tiketi zitauzwa kwa shilingi elfu
kumi na kuongeza kuwa wanamuziki watakaoshiriki onyesho hili
wamejipanga kutoa burudani kisawasawa na kukata kiu ya wapenzi wa muziki
wote Nchini.
Alisema tiketi za onyesho hilo zitauzwa katika vituo mbalimbali
Nchini yakiwepo maduka ya Vodacom Tanzania,Pia zitapatikana kupitia
huduma ya M-Pesa,Katika kuwapunguzia washabiki usumbufu wa kupanga
misururu ya kununua tiketi za onyesho hilo pia zitauzwa kwa kupitia
huduma ya M-Pesa bila kuwepo na makato yoyote ya kutumia huduma hiyo
ambapo watakaonunua tiketi kwa huduma hiyo kutakuwepo na utaratibu
maalumu wa kuingia kwenye onyesho cha muhimu ni kutunza namba zao za
kumbukumbu ya mhamala wa malipo.Jinsi ya kujipatia tiketi kwa njia ya
M-PESA mteja anatakiwa kupiga *150*00# na kuchagua LIPA KWA M-PESA
2. Chagua MANUNUZI
3. Chagua JEMBEKA FESTIVAL
4. Weka namba ya kumbukumbu – 200200
5. Weka kiasi – 10,000
6. Weka Namba yako ya siri na kwa wale wa tiketi za VIP namba ya kumbukumbu ni 200100 bila malipo yeyote yale.
Kwa msaada wa kununua tiketi, piga BURE namba 0800 71 0040
No comments:
Post a Comment