HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Wednesday, 4 May 2016

Tecno waja na simu mpya Boom J8

Boom J8 ni kifaa kipya kabisa kutoka TECNO ambacho kimekuja mwishoni mwa mwezi wa April mwaka huu. Smartphone zimeendelea kurahisisha maisha ya watumiaji wake kila kukicha.





1



Najaribu kufikiri kama maisha bila mziki yangelikuwaje, ama mziki ungekuwepo lakini usingekuwa na kiungo chochote kile yaani mashairi tupu bila mdundo.
TECNO inafahamu kitu ambacho wajanja wote wanakitaka kuongezewa katika mziki ndio maana ikaja na Boom J8 Smartphone ya kijanja iliyotengenezwa maalumu kwa ajili ya wapenda mziki. Boom J8 imetengenezwa kuzingatia mahita yako yote mziki katika maisha yako ya kila siku.
Hebu tujaribu kuitupia jicho Smartphone hii ambayo imetokea kuwa gumzo mjini. Katika kitu cha kwanza ambacho TECNO wameua katika simu hii ni kuiuza pamoja na Headphones mpya kabisa ambazo zinakuja na smartphone, headphone hizi ni maalumu kwajili ya Boom J8 tu ndio maana zinauzwa pamoja na simu hii. Headphone hizi zinafaamika kama Boom Headphones.
Lakini pia Smartphone hii inekuwa ya kwanza kuja na Operating System mpya ambayo itakuwa inapatikana katika smartphone za TECNO peke yake. HiOS ni OS ambayo inaifanya Boom J8 kuwa ya kipekee na tofauti kabisa na OS nyingine ulizozizoea.
Katika HiOS mtumiaji anaweza kubadilisha Theme katika smartphone yako na kuifanya kuwa na mwonekano wa toauti kabisa na simu nyingine.
Boom J8 sasa inapatikana katika maduka yote mjini unaweza kuipata kwa bei nafuu Zaidi. Wahi madukani ujinyakulie chombo ambacho kitakata kiu tako ya mziki.

No comments:

Post a Comment