HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Sunday 15 May 2016

VIDEO: Mbunge aliyempongeza Diamond Platnumz

May 13 2016 ilikuwa ni zamu ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017 kiwango kilichoombwa ilikuwa ni Sh. 20,326,176,000 ambapo kati ya hizo, fedha za matumizi ya kawaida ni Sh. 17,326,176,00 Katika kipindi cha kupokea michango ya maoni kutoka kwa Wabunge, Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga akaguswa na harakati za staa wa Bongo flava Diamond Platnumz… >>’Ingekuwa amri yangu tungechonga sanamu la Diamond tukaliweka kwenye mnara wa Askari, ule mnara tumeuchoka. Ametufikisha mbali naameitangaza nchi yetu huko mbele‘ ‘Serikali hatuna mpango wowote wa kuwasaidia wanamuziki, wanapenya wenyewe tunaenda kukutana nao mbele na sisi tunajifanya kuwasaidia. Yuko wapi Mr. Nice?,hatujawawekea mfumo mzuri, ninaongea haya nikiyamaanisha’ Unaweza kumcheki kwenye hii video hapa chini…

No comments:

Post a Comment