Said Salim Awadh Bakhresa.
KATI ya
miaka ya 1960 hadi 1980, mtu kuwa tajiri alionekana ni hatari kwa taifa,
tena mali zake alizimiliki kwa kificho, vinginevyo angeitwa mhujumu
uchumi. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, taratibu sera za kibepari
zinatawala, ujamaa unapewa kisogo.
Mtu kama
ni mbunifu, ana nidhamu ya kutofuja pesa na anafanya kazi sana kwa nini
asiwe tajiri? Utandawazi unasaidia ndiyo maana leo tunaweza kuwatambua
mabilionea wakubwa ambao wanastahili pongezi kwa hatua walizopiga.
Tusisahau kuwa wanaibeba nchi kwa ulipaji kodi.
1. SAID BAKHRESA
Jina lake
kamili ni Said Salim Awadh Bakhresa. Jarida la Forbes mwaka jana,
lilimuorodhesha miongoni mwa matajiri 40 Afrika kwamba anamiliki utajiri
wenye thamani ya dola milioni 620 (karibu shilingi trilioni moja). Hata
hivyo, inadaiwa kuwa tabia ya usiri wa Bakhresa inafanya mali zake
zisijulikane sana, ila ni tajiri zaidi ya kiwango hicho.
Ndiye
mmiliki wa makampuni ya Bakhresa yanayotoa bidhaa zenye chapa ya Azam
ambazo zinauzwa nchi mbalimbali Afrika. Ana viwanda vya nafaka na
vinywaji, vyombo vya usafiri wa majini, uuzaji wa chakula, bidhaa za
plastiki na kadhalika. Ndiye mmiliki wa Klabu ya Azam FC.
2. GULAM DEWJI
Huyu ni
baba wa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’. Jarida la
Forbes mwaka jana lilimtaja kuwa na utajiri wenye thamani ya dola
milioni 560 (karibu shilingi bilioni 900). Mafanikio yake kibiashara
yalianza mwaka 1970. Kiwanda chake cha 21st Century Textiles, kinatajwa
kuwa moja ya viwanda vikubwa vya nguo Afrika.
3. ROSTAM AZIZ
Inadaiwa
anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 420 (shilingi bilioni
672). Anamiliki karibu asilimia 40 ya hisa Kampuni ya Vodacom Tanzania.
Ni mmiliki wa Kampuni ya Caspian inayohusika na uchimbaji wa madini na
ukandarasi nchini Tanzania, nchi kadhaa za Afrika na Asia.
4. DK. REGINALD MENGI
Anatajwa
kumiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 280 (karibu shilingi
bilioni 450). Ni mmiliki wa kundi la makampuni ya IPP, yanayomiliki
vyombo vya habari, viwanda, migodi ya dhahabu, Tanzanite na kadhalika.
5. ALI MUFURUKI
Utajiri
wake unatajwa kuwa na thamani ya dola milioni 110 (shilingi bilioni
176). Ni mmiliki wa kundi la makumpuni ya Infortech Investment,
inayomiliki maduka yanayouza vitu vya rejareja Tanzania na Uganda.
Vilevile ana vitega uchumi vingine.
6. MUSTAFA SABODO
Ni
mfayabiashara mkubwa sana nchini anayemwaga mamilioni kwa misaada.
Wakati wa kuanzishwa kwake, aliipa Taasisi ya Mwalimu Nyerere shilingi
milioni 800, akasaidia shilingi milioni 100 katika mradi wa kustawisha
mimea jamii ya kunde. Vilevile alikipa Chadema shilingi milioni 300.
Inadaiwa kuwa utajiri wake unazidi shilingi bilioni 100. Kampuni yake ya
Khoja Shia Itnasheri Jamat (KSIJ), ndiyo yeye tenda ya kujenga maeneo
ya maegesho ya magari Posta, Dar es Salaam, mradi wenye thamani ya
shilingi bilioni 5.6.
7. ABDUL-AZIZ ABOOD
Kiwango
chake cha utajiri hakiwekwi sana wazi lakini anatajwa kuwa miongoni mwa
mabilionea 10 wanaotikisa nchi kwa sasa. Anamiliki viwanda kadhaa mkoani
Morogoro, vyombo vya habari, Abood Radio na TV. Anamiliki mabasi ambayo
yanafanya safari zake kati ya Morogoro, Mbeya na Dar es Salaam. Ni
Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM).
8. MICHAEL SHIRIMA
Ni
mmiliki mkuu wa Shirika la Ndege la Precision ambalo linafaya safari
zake ndani ya Tanzania pamoja na nchi mbalimbali za Afrika. Ana asilimia
tano ya hisa katika Beki ya I&M (Tanzania), vilevile ni memba
katika bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo yenye thamani ta shilingi
bilioni 200. Hisa zake Precision ni asilimia 42.91.
9. YUSUF MANJI
Kiwango
halisi cha utajiri wake bado hakifahamiki lakini anafahamika kama mmoja
wa mabilionea wakubwa nchini Tanzania. Ni mmiliki wa makampuni ya
Quality Group na majengo ya Quality Centre, Quality Plaza na kadhalika.
Ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na utajiri wake umeifaya timu
kutotetereka tangu alipoanza kuiongoza.
10. MOHAMMED DEWJI
Baba yake
anashika nafasi ya pili katika orodha hii. Dewji au Mo kama anavyoitwa
na wengi, anatajwa kuwa bilionea nambari moja katika orodha ya
mabilionea vijana Afrika (orodha hiyo tuliitoa wiki iliyopita). Ni
mmiliki wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL)
ambayo inatengeneza faida ya shilingi bilioni 136 kwa mwaka
No comments:
Post a Comment