Kila wakati wengi wetu katika maisha, ni watu wa kujiwekea malengo. Mara nyingi huwa tunaweka malengo haya, kwani kwa kujiwekea malengo hayo ndiyo hutuongeza na kutuhakikishia kule
tunakotaka kufika kimafanikio. Kwa kujua hili, karibu kila mtu msaka
maendeleo, kwake malengo huwa ni kitu cha lazima sio cha kuuliza tena.
Lakini
hata hivyo, pamoja na kujiwekea malengo mazuri, kwa bahati mbaya sana
tena wengi wetu huwa bado hatuyafikii malengo hayo. Hapo ndipo maswali
mengi sana ya kwanini huanza kuibuka vichwani kwetu? Kama mambo ni hivyo
usikate tamaa, Kwa kufatilia makala haya utajifunza juu ya mambo muhimu
yatakayokusaidia kufikia malengo yako.
1. Yajue malengo yako vizuri.
Huwezi
kufanikiwa kama huyajui malengo yako vizuri. Ni lazima malengo yako
yawe ya wazi kwako. Ikiwezekana yaandike vizuri kwenye karatasi nayaweke
sehemu inayoonekana. Kwa mafano kama lengo lako ni kufanya biashara ya ‘stationary’ liandike lengo hilo mahali na lionekane. Kama pia lengo lako ni kufungua duka weka wazi lengo lako kwa kuliandika.
Watu
wengi mara nyingi wanashindwa kufikia malengo yao kwa sababu malengo
yao yanakuwa sio wazi sana. Siku zote mawazo yetu ya ndani hutusaidia
kufikia malengo yetu, kama malengo hayo yana eleweka. Kinyume cha hapo,
utakaa sana kusubiri malengo yatimie lakini wapi. Hivyo siri ya kufikia
mafanikio jitahidi kuweka malengo yako wazi.
HAKUNA CHA KUKUZUIA KWENYE MAFANIKIO UKIAMUA. |
2. Jitoe kikamilifu.
Siri
ya mafanikio ni kujitoa kikimalifu kwa kile unachokifanya. Hata malengo
yako ambayo umeshajiwekea na yako wazi ili kuweza kuyafikia ni lazima
ufanye juu chini kujitoa kikamilifu na wala sio nusunusu. Ikiwa utakuwa
unayaendea malengo yako, huku ukiwa hujaamua kujitoa kikamilifu tambua
ikatokea umeshindwa usishangae hapo kwa hilo.
Kwa
kuwa unanajua malengo yako nini, kama kuna kazi unatakiwa kuifanya
ifanye kweli kwa nguvu zako zote bila kuchoka. Weka juhudi na maarifa
yako yote na kuhakikisha unajitoa kweli. mafanikio yako hayatakuja
kirahisi eti kwa kufanya kazi kilegevu. Jitoe kwa kupiga kazi kwelikweli
mpaka kieleweke.
3. Kamilisha majukumu yako kila siku.
Unaweza
ukawa unayajua malengo yako na umejitoa kikamilifu, lakini huwezi
kuyafikia malengo yako kama kila wakti unakuwa hukamilishi zile kazi
zinazotakiwa kukusaidi kuyafikia malengo yako. Hapa sasa ndipo
unapotakiwa kujilazimisha na kuhakikisha kila jukumu ulilonalo
unalikamilisha kwa siku husika.
Kwa
mfano kama wewe ni mfnyabiashra ulitakiwa kupga mahesabu Fulani ya
kukusidia, fanya hivyo bila kuacha. Halikadhalika akama wewe ni
mwandishi na umejipangia kuandika kurasa mbili kwa siku, pia fanya hivyo
bila kuacha wala kuahirisha. Kwa kukamilisha majukumu yako kila siku
itakusaidia kufikia malengo yako kuliko ambavyo ungefanya mambo
nusunusu.
4. Yagawanye malengo yako.
Malengo
yoyote ulinayo yanaweza kufikika. Haijalishi malengo hayo ni makubwa
kivipi lakini uwezo wa kuyafanikisha upo, ikiwa tu lakini utafuata hatua
za kuyakamilisha malengo hayo. Pengine unajiuliza kivipi au nitawezaje
kuyakamilisha malengo yangu makubwa? Ni rahisi tu na hata wewe unaweza.
Kulielewa
hilo vizuri ngoja nikupe kisa kimoja moja ambacho kinaelezea siku moja
fisi mkubwa alimkuta fisi mdogo akimla tembo. Fisi Yule alivyoona vile
alicheka sana na kumuuliza utamaliza lini? Fisi Yule mdogo alimwambia
nitamla kidogo kidogo mpaka ataisha. Kwa kutumia mfano huo hivyo, ndivyo
unavyotakiwa na wewe kufanya kwa malengo yako makubwa. Unajiona una
malengo mkubwa yagawe vipande vipande mpaka uyafikie..
5. Tafuta msaada.
Ni
rahisi kuyafikia malengo yako, kama utatafuta msaada wa kukusaidia
kuyafikia malengo hayo. Acha kung’ang’ania kukamilisha malengo hayo
ukiwa peke yake. Yaangalie malengo yako yana husu nini kisha baada ya
hapo jiulize je, ni mtu gani au watu gani ambao wanaweza kunisaidia
kukamilisha malengo haya.
Kwa
kujua watu ambao watakusaidia kukamilisha malengo yako itakusaidia sana
kushirikiana nao kwa ukamilifu na kwa ubora wa hali ya juu hadi kufikia
mafanikio yako. Tambua na elewa sio kwa sababu malengo ni yako, hivyo
unatakiwa kuyakamilisha mwenyewe, hapana. Tafuta kile unachokosa, kisha
omba msaada.
6. Kuwa chanya wakati wote.
Kuna
wakati tunapokuwa tunajiwekea malengo huwa tunakutana na changamoto
nyingi sana ambazo zinatukatisha tamaa. Sasa hali hii inapokutokea ni
vyema ukajitahidi ukawa chanya wakati wote. Acha kukataa wala kujiona
hufai, endelea kusonga mbele kati kati ya changamoto hizo ulizonazo
wewe.
Kuwa
chanya wakati unatafuta mafanikio inalipa sana. Tuchukulie kwa mfano
unafanya biashara halafu ukapata hasara, hapo unafanyaje? Utaacha au
itakuaje? Jibu ni kuendelea na safari ya mafanikio kwa kutambua kwamba
hiyo nayo ni hatua ya mafanikio pia. Ndiyo maana tunasema ni muhimu na
lazima kuwa chanya ili kuyafikia mafanikio yako.
7. Kuwa tayari kuyapitia malengo yako kila wakati.
Pamoja
na kwamba umejwekea malengo vizuri, umejitoa kabisa kwenye malengo
hayo, lakini hutakiwi kusahau kabisa kuyapitia malengo yako. Ni muhimu
kuyapitia tena na tena malengo kwa kutambua wapi ulipofikia, nini
kinachokukwamisha na ufanye nini ili uweze kusogea hapo ulipo kwa kasi
zaidi.
Watu
wengi wenye mafanikio wanayapitia malengo yao. Wanapita malengo yao
asubuhi, wanapitia malengo yao mchana, wanapitia malengo yao jioni.
Picha kamili ya malengo yao inakuwa ipo kichwani mwao tayari. Hiki
ndicho kitu ambacho unatakiwa ukifanye hata wewe. Pitia malengo yako
kila wakati ili yaumbieke vizuri na itakusaidia kuyakamilisha.
8. Jifunze kufurahia mafanikio kila hatua unayopitia.
Pamoja
na kujiwekea malengo yetu makubwa, lakini kumbuka kuna yale malengo
yetu madogo madogo ambayo huwa tunayashinda. Inapotokea umefanisha jambo
fulani, hata kama kwako ni dogo ni vyema ukajifunza kulifurahia.
Furahia mafanikio yako siku hadi siku kwa jinsi unavyoyapata. Hiyo
itakupa nguvu ya kufanikisha mambo mengine.
Kama
kweli una nia njema ya kufikia mafanikio makubwa, basi hayo mambo ni ya
msingi sana katika kukusaidia kufikia malengo yako makubwa
uliyojiwekea. Jukumu lako kubwa ni kuhakikisha unayaweka kwenye vitendo
mambo hayo. Na kwa kufanya hivyo basi utaweza kufikia malengo yako na
kutakuwa hakuna wa kukuzuia.
Nikutakie siku njema na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati. Usikose kuwaalika wengine waweze kujifunza kupitia makala tunazozitoa hapa.
No comments:
Post a Comment