Ndoto
sio tu kile kitu unachokiona uwapo usingizini bali pia ni kile
unachotamani kukiona uwapo macho na kinakunyima usingizi.Ni mara nyingi
miongoni mwetu tumekuwa na ndoto kadhaa.Kupunguza mwili,kupata
kazi,kununua kiwanja,kuoa,kusomesha,kufanya biashara na
mengineyo.Tuwazapo ndoto za aina hii dhahiri tunafungua vichwa kuwa
vielevu,tunavisaidia kuwa komavu,tunaviwajibisha kuwa na busara
halikadhalika hatuviepushi kuwa imara .Na njia kuu ya kutimiza ndoto
yako ni pamoja na kufanikisha za wengine.Huku ukichukua masomo mhimu
kutoka katika usumbufu na urahisi mmoja aliopitia.Ikiwa hapo juu tumeona
ndoto ni kama mizizi inayoshikilia shina na matawi ya maisha yetu kwa
maana zinagusa afya,ajira,makazi,familia,na uchumi, ni vigumu sana
kutenganisha binadamu na ndoto,ndoto na binadam.Swali la msingi ni nini
kifanyike ili ''kugarantee'' ndoto zetu? .Yapo mambo mengi ya kufanya
ila hapa nakushauri kwa haya mawili matatu ya kuufanya ili ndoto itimie
na kudumu milele.
1.ANZA HAPO ULIPO
Namna
ndogo ya kukaribisha ndoto kubwa ni pamoja na kuanza kuona kila jambo
gumu ni jepesi, kila linaloshindikana linawezekana.Na namna
tulivyo leo ni matunda ya maamuzi tuliofanya jana.Inawezekana
tunasubiri sana,hatuamini mazingira yanayotuzunguka,au watu
tunaoishinao.Lakini ukweli ni kuwa maisha ni popote.Dangote ni bilionea
mwenye heshima duniani anayetokea Afrika sehemu iliyowahi kuitwa ni bara
la giza.Facebook ni mtandao mkubwa wa kijamii ulimwenguni lakini uliogunduliwa huko mabwenini.
2.TUMIA ULICHONACHO.
Muumbaji
wetu ni wa ajabu sana ,wakati wa kuumba binadamu hakumnyima cha
kufanya.Kama huna mikono una macho,kama huna macho una miguu kama huna
miguu una mikono,kama huna mikono una mdomo na kama huna kinywa basi una
akili.Akimaanisha Usipocheza kikapu kama Jordan utakuwa Goal keeper
kama Kaseja.Usipokuwa na Sauti ya kuimba kama Steve Wonder utakuwa
mzungumzaji mzuri kama Nyerere.Na usipokuwa ''genius'' kama Einstein
utakuwa msomi kama profesa Lipumba.Usipokua mwandishi kama Shakespear
utakuwa mtunzi kama Shaban Robert.Tumia ulichonacho na ndoto yako
itimie..
3.FANYA UNACHOWEZA.
''Kwani
wao weweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini?''Ni swali alilouliza
Juma Nature msanii mwenye ushawishi katika mziki wa kizazi kipya
.Kinachopelekeaa mwingine kuweza ni mjumuiko wa makosa na masahihisho
wanayofanya.Hutenda kiasi kidogo leo,kiasi kingine kesho na kingine tena
kesho kutwa.Jumla ya utendaji huu kwa wiki,mwezi,mwaka ni mkubwa kiasi
cha kutisha mtu mwingine .Na kila hatua mpya inakuwa bora kuliko
iliyopita.
4.USIVUNJE SHERIA.
''Ukivunja
sheria utapigwa tu'' Mizengo Pinda,waziri mkuu mstaafu aliwahi
kusema.Hivyo akati tukitegemea neema kuu ndani na nje ya ndoto zetu
hatuna budi kuheshimu kanuni na taratibu .Hasa zile zinazoongoza
nchi,zinazolinda mtu na kutetea uhuru wa kila mmoja.katika umiliki wa
rasilimali.Sitegemei utimize ndoto kwa njia ya
wizi,dhuruma,ukabaji,unyang'anyi na njia nyingine zisizo halali.
No comments:
Post a Comment