Bahati ni ndoa ya vitu viwili: maandalizi na
fursa.Fursa ni msingi wajambo moja,nafasi .Nafasi ni mahusiano ya mambo
matatu;nia uwezo na utekelezaji.Utekelezaji unahitaji jambo moja,
mtu.Mtu ni nafsi inayoweza kugawanywa katika utatu, mimi,wewe na
yule.Palikuepo na mtu mmoja alie amini katika bahati,fursa,nafasi, na
utekelezaji .Huyo mmoja alikuwa kiongozi.Uongozi wake ulijaa utani.Hata
moja ya kauli yake pendwa ilikuwa ni hii.''Ndugu wana nchi msidharau
vitu vidodo,vitu vidogo vinaumiza,kama mnabisha jaribu kukalia sindano''
.Halaiki ilikufa kwa mbavu baada ya huu utani.Ukitaka kuamini vitu
vidogo ni muhimu vinaendesha dunia,na ukivithamini utafurahia ,hautaumia
ungana nami kwenye hizi stori zifuatazo
Hakuwahi kujiona kama mpiga ngumi,au bingwa
wa makonde kimataifa.Mpaka pale alikumbwa na mkasa mdogo sana.Mohamedi
Ali akiwa kijana mdogo miaka kama kumi na kitu ivi.Aliibiwa baiskel
anayoipenda .Na akaripoti kwa askari kuwa akimpata mwizi atampiga.Askari
alimwambia atamwajibishaje mwizi yule wakati hana uwezo wa
kupigana.Basi ikabidi askari amfundishe Mohamedi Ali kuchapa
masungwi.Baada ya kuiva hakumtafta mwizi ila akaingia kwenye mashindano
ya ngumi
.
2.MOHAMMED DEWIJ
Safari yake ki siasa ilianza baada ya kuona
tukio dogo mkoani mwake Singida.Anasimulia''Nimetoka(Singida mjini) km 6
nakutana na mzee mmoja,kulikuwa kuna maji ya njano chini ,alikuwa na
ndoo na sinia,amechuchumaa akiteka maji nakutia ndani ya
chombo.Nikamsalimia mzee Shikamoo,unafanya nini hayo maji,akasema haya
maji ndio tunakunywa sisi.Sikumwamini hadi pale nimefika kwake na kuona
watoto wakinywa maji yale yale ,mzee akanisihi MO,kwa nini usigombee
ubunge?''Na Harakati zikaanzia hapo akiwachimbia wananchi wa Singida
visima akiwa kama mbunge.
3.JUX
Licha ya kupenda kun'gaa ,kupendeza na
kusogolea wanamziki na mziki ,Juma jux hakuwahi kufikiri kama ni
mwimbaji.Alikuwa anafanya hip hop ila baada ya tukio la bahati au dogo
kumtokea .Siku ile imeleta mwimbaji anaetambulika kwa
sauti,nyimbo,mavazi na Video kali Afrika Mashariki.Na hapa jux mwenyewe
anasimulia .
''Tulienda studio na Cyril,Cyril alitakiwa
kufanya collabo na Makamua .Makamua alikuwa msanii mkubwa.Basi(Cyril)
akampigia Makamua,Makamua akadai atakuja, tulichoma sana mahindi
pale(tulikaa sana).Kuanzia kama saa moja mpaka saa tano tano.Maneke(
producer wa muziki) akawa kaweka ile Beat.Ile beat imewekwa mie nikawa
kama naimba tu unajua mzuka wa studio.Maneke akasikia naimba,akasema ebu
imba tena,nikaimba.Akanambia mbona unaweza kuimba kwa nini
unachana(kurap).Saa izo naogopa kinoma naogopa ile mic sana,sio nilikuwa
naogopa kuimba,nilikuwa naogopa kusikiliza nyimbo yangu mwenyewe
kwenye redio,nilikuwa naona aibu sana.Akasema(Maneke) unaweza kuimba
jaribu.Nakumbuka ndo mara ya kwanza naingia booth kurekodi''
No comments:
Post a Comment