Kwa kawaida wanyama wakali kama Simba,
Chui, na wengine huwekwa chini ya usimamizi mkali endapo kukiwa na
hatari ya kudhuru binadamu ama wanyama wanaowazunguka. Ila taarifa za
kuwahukumu simba watatu kifungo cha maisha baada ya kugundulika wamemla
mtoto wa miaka 14 huko India kimeshangaza wengi
Kwa kawaida tumezoea kuona Simba akiuliwa kama ikitokea kamshambulia binadamu lakini sio kufungwa, ila India
wamefikia maamuzi tofauti kidogo ya kuwafungia kifungo cha maisha Simba
watatu kutokana na wananchi wa eneo hilo kulalamika kutokea kwa
matukio hayo.
Simba hao watatu,
wawili wakiwa wakike na dume mmoja, walimshambulia mtoto aliyekuwa
amelala nje ya nyumba kwenye bustani katika hifadhi ya taifa ya Gir Gujarat India. Mtoto huyo atakuwa mtu wa tatu kuliwa na Simba
tangu April 2016 hali ambayo ilisababisha wananchi wa eneo hilo kuiomba
serikali ichukue hatua ili kutokomeza matukio ya aina hiyo.
No comments:
Post a Comment