Monday 27 June 2016
Video: Beyonce na Kendrick Lamar walivyotumbuiza ‘Freedom’ kupinga ubaguzi
June 26 ilikuwa ni siku ya utoaji wa tuzo za BET zinazoandaliwa na kituo kikongwe cha burudani nchini Marekani, Black Entertaiment Television, BET. Zililifanyika kwenye ukumbi wa Microsoft Theater, Los Angeles.
Ukiacha utoaji wa tuzo hizo huwa na wasanii mbalimbali wanaotumbuiza mbele ya maelfu ya watazamaji waliohudhuria utoaji wa tuzo hizo.
Performance iliyowashangaza wengi ni ile ya staa wa pop na R&B hit maker Beyonce alipopanda jukwaani na kutumbuiza single yake inayofahamika kama Freedom aliyomshikirisha rapper Kendrick Lamar. Ni wimbo ambao maudhui yake yamejaa hisia zenye mrengo wa kisiasa kutokana na kuripotiwa matukio mengi ya mauaji ya watu weusi yaliyofanywa na polisi nchini Marekani kwenye miaka ya hivi karibuni.
Kwa kuonesha kuwa wanapinga ubaguzi wakati madancer wa Beyonce wanapanda jukwaani walisindikizwa na sauti ya mwanaharakati wa haki za binadamu duniani, Hayati Martin Luther King Jr ambapo sehemu ya hotuba yake maarufu iliyopewa jina ‘I Have A Dream’ ilisikika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment