HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Friday, 8 July 2016

‘Facebook sasa kutuma na kupokea fedha bure’


Moja ya habari zilizoandikwa kwenye magazetini hii kwenye gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘Facebook sasa kutuma  na kupokea fedha bure’
Gazeti hilo limeandika kuwa utandawazi unazidi kushika kasi ambapo kadri siku zinavyozidi kwenda mambo yanabadilika. Ndiyo maana sasa hivi kuna mambo mengi ambapo licha ya kuwa Tanzania mambo mengine yanachelewa kutufikia, lakini siku moja tutatumia huduma hizo kama ilivyo kwa mataifa yaliyoendelea kiteknolojia.
Kila kukicha mmiliki wa mtandao huo, Mark Zurgbeck amekua na mawazo mapya ya kuvutia kwa wateja kwenye huduma yake hiyo kwa kubuni mambo mbalimbali yanayowagusa wateja wake.
Kama wewe ni miongoni mwa wanaotumia mtandao huu kupitia App ya Messenger tambua kuwa siku chache zijazo utakua na uwezo wa kufanya malipo ya bidhaa au kutuma na kupokea fedha kupitia mtandao huo.
Huduma hiyo iliyobatizwa jina la PayPal itakua ikitumika kama ilivyo ile ya simu japo cha kufurahisha hapa ni kuwa huduma hiyo haitakuwa na makato ya aina yoyote kama ilivyo kwa mitandao ya simu, isipokuwa tu itawahusu watumiaji wa Debit Card pekee na walio na umri wa miaka 18 na kuendelea.
Huduma hiyo itaanza kutumika nchini Marekani  ambapo mtu atatuma na kupokea fedha huku ikitarajiwa kusambaa kwenye mataifa mengine.
Namna ya kutumia huduma hii fungua sehemu yako ya Chatting kisha chagua More halafu nenda kwenye alama ya $ halafu nenda palipoandikwa ‘Pay’ kisha unamalizia na sehemu iliyoandikwa ‘Add New Debit Card kisha utaulizwa kiasi unachohitaji  kulipia utaingiza na kuletewa risiti inayoonyesha kuwa malipo yamekamili

No comments:

Post a Comment