HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Friday 8 July 2016

Harmonize: Chumba cha video ya ‘Matatizo’ ndicho nilichokuwa nimepanga


Harmonize amefafanua kuwa chumba kinachoonekana kwenye video ya ‘Matatizo’ ndicho chumba chake alichokuwa anakaa huko Kiwalani kabla hajawa staa.
13092352_982346051872778_572349746_n
Akiongea na Magic FM Jumanne hii, Harmonize alisema kuwa kuimba nyimbo za matatizo uliyowahi kupitia zinasaidia kuwa inspire watu japo wengine wanadai kuwa kufanya hivyo ni ushamba.
“Muda mwingine kueleza matatizo uliyoyapitia ni kama ushamba hivi, muda mwingine kueleza vitu ulivyopitia ni kitu kizuri kwa kuwa unawa inspire vijana wengi sana ambao wapo mtaani hata wazee pia waliokaribia kukata tamaa,” alisema Harmonize.
“Kwenye video ya matatizo kwa asilimia kubwa vyote nilivyoimba ni historia yangu kabisa. Hata kile chumba nilichoshoot video ndio chumba nilichokuwa nimepanga wakati nakaa Kiwalani,” aliongeza.
Aidha Harmonize aliongeza kuwa wakati anakaa kwenye chumba hicho aliweka kapeti lake la bei rahisi na kigodoro pekee.

No comments:

Post a Comment