Sunday, 3 July 2016
Izzo Bizness aanzisha kundi ‘The Amazing’ na mrembo huyu
Kuna kundi jipya mjini – The Amazing. Kundi hili linaundwa na rapper Izzo Bizness na muimbaji aliyekuwa na makazi yake nchini Marekani mwenye asili ya Tanzania, Abela.
Izzo amesema kabla hata ya kuja na wazo la kuanzisha kundi hilo, alikuwa akichat na Abela aliyekuwa Marekani na kumweleza kuwa baba yake ni shabiki mkubwa wa nyimbo zake pamoja na maisha anayoishi rapper huyo wa Mbeya.
“Abela baba yake unajua ni Mtanzania mama yake ndio Msweden nafikiri kwahiyo yeye ni Mtanzania na kwao ni Bukoba lakini hapa Dar es Salaam pia ana ndugu zake,” anasema Izzo.
“Alikuwa na plan za kuja kukaa Dar muda mrefu na kwakuwa ni Mtanzania so hakukuwa na ugumu wowote kwa safari yake kuja hadi huku.” Ameiambia Bongo5 kuwa jina la The Amazing lilikuja baada ya wao kukaa na kujadili na kutaka kupata jina rahisi kwa watu na lililopo mdomo kwa wengi.
“Na hata tukikaa wawili picha ambayo unaona ni amazing kwasababu tunavyoonekana na nini hata na muziki ambao tunafanya,” amesisitiza.
Izzo anasema watu wategemee vitu tofauti kutoka kwao kwasababu kundi linaundwa na jinsia mbili tofauti na ladha zao nyingi zitakuwa ni hip hop, kitu ambacho anaamini hakipo Bongo.
“Sisi tumeamua kuja na taste ya hip hop lakini kundi lina mwanamke na mwanaume.”
The Amazing wataachia video ya wimbo wao wa kwanza uitwao Dangerous Boy Jumatano ijayo. Wimbo umetayarishwa na producer Dupy wa Uprise Music huku video ikiongozwa na kampuni ya Focus Films chini ya muongozaji Nick Dizzo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment