Headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, UTayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya habari zilizoandikwa kwenye magazeti ni hii ya kwenye gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘TCU YATOA SIFA MPYA KUJIUNGA VYUO VIKUU’
Gazeti hilo limeandika kuwa Tume ya vyuo vikuu Tanzania ‘TCU‘
imetangaza utaratibu mpya kwa watahiniwa wa mwaka mpya wa masomo wa
2016/2017 wanaochukua shahada, huku wanafunzi wengi wakiwa hatarini
kukosa nafasi ka kukosa sifa na vigezo.
Utaratibu
huo mpya umekuja ikiwa ni miezi miwili sasa tangu kutumbuliwa kwa
watendaji wa tume hiyo kutokana na kudahili wanafunzi wasio na sifa na
kusababisha kupewa mikopo na bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya
juu.
Sifa hizo zilizowekwa mapema wiki hii katika tovuti ya TCU na kurudiwa jana, Moja
ya sifa zinazotakiwa katika udahili wa mwaka huu wa masomo ni wahitimu
wa kidato cha sita waliomaliza kabla ya mwaka 2014 kuwa na ufaulu wa ‘D
mbili’ pointi 4.0. Mchanganuo ulionyesha kuwa pointi hizo zinatokan na
ufaulu wa A=5; B=4; C=3; D=2; E=1.
Taarifa
hiyo iliyoonyesha kuwa wahitimu wa kidato cha sita kwa mwaka 2014 na
2015 ili wawe na sifa za kudahiliwa z, watatakiwa kuwa na alama za
ufaulu wa ‘C mbili’ pointi 4.0 kupitia mchanganuo wa A=5; B+=4; B=3; C=2; D=1.
Kupitia
tovuti hiyo iliyoonyesha kuwa wahitimu waliomaliza kidato cha sita kwa
mwaka huu watahitajika kuwa na ufaulu wa alama ‘D mbili’ 4.0 kupitia
mchanganuo wa A=5; B=4; C=3; D=2; E=1.
Mbali na
sifa hizo, watakaodahiliwa ni wale ambao pia watakuwa na utambulisho wa
sifa za kielimu za kidato cha nne ambazo ni kuanzia alama nne ambazo ni D
na kupanda juu katika mchanganuo wa alama za ufaulu wa B+, ikiwa A=75-100, B+=65-74, B=50-64, C=40-49, D=35-39, F=0-38.
Sifa
nyingine zinazotakiwa ni wenye cheti cha NVA daraja la tatu pamoja na
ufaulu wa si chini ya alama nne au sifa nyingine zinazokaribiana na
hizo, ikiwa ni pamoja na zinazotambuliwa na baraza ka Taifa la mitihanai
‘NECTA’ na mafunzo ya ufundi ‘VETA’
Watahiniwa
hao watatakiwa kuwa na angalau GPA ya 3.5 kwa stashahada ‘NTA’ daraja
la sita au wastani wa B kwa cheti cha ufundi ‘FTC’ katika mchanganuo wa
alama A=5, B=4, C=3 na D=2 au wastani wa daraja la B+
kwa wenye stashahada za ualimu au wastani wa daraja B+ kwa kitengo cha
afya kama tabibu wa magonjwa ya binadamu na nyingine au cheti na
stashahada nyinginezo.
Sifa nyingine zinazoangaliwa katika udaahili huo ni kuwa na ufaulu wa daraja la pili kwa wenye stashahada zisizokuwa za NTA.
No comments:
Post a Comment