Najua kama ni mtumiaji wa usafiri
wa ndege utakuwa umekutana na taratibu za abiria kuzima simu wakati
ndege inataka kupaa na kutua ila huenda ikawa hufahamu ni kwanini
haswa unatakiwa kufanya hivyo, na inawezekana ulishajiuliza pia ina
maana usipozima unaweza kusababisha ndege kupata ajali? jibu ni Hapana, isipokuwa unaweza kusababisha muingiliano wa mawasiliano kati ya rubani na waongozaji.
Vibrations au miungurumo ya simu na
vifaa vingine vya electronics vinahusika kwa kiasi kikubwa kuvuruga
mawasiliano mazuri kati ya rubani na wanaomuongoza, hivyo huwa
tunashauriwa kuzima simu na vifaa vingine vya electronics wakati wa
kupaa na kutua kwa ndege. Hiyo ni moja kati ya sababu kuu zilizotajwa
kuhusiana na swali la ”Kwanini tuzime simu wakati ndege inaporuka na
kutua”?.
No comments:
Post a Comment