HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Sunday, 18 September 2016

Kurekodi na Trey Songz ni mwanzo wa kutimiza ndoto yangu ya kushinda Grammy – Vanessa Mdee




vanessa-8

Na sasa anaamini kuwa, mwanzo wa kukaribia kuiishi ndoto hiyo umewadia. Vee Money, ni mmoja wa wasanii wa Afrika, waliochaguliwa kurekodi wimbo na mshindi wa Grammy na nyota wa RnB nchini Marekani, Trey Songz. Shukrani kwa kipindi cha Coke Studio Africa (International Week) msimu wa 4, kinachomdondosha staa huyo.
Akiwa pia anawania tuzo ya Loeries za Afrika Kusini kwa kazi yake ya video bora, Niroge, Vanessa anaungana na Rema Namakula (Uganda), Yemi Alade (Nigeria), Neyma (Mozambique), Serge Beynaud (French West Africa), Lij Michael (Ethiopia), Stonebwoy (Ghana), Nyashinski (Kenya) na Emtee (South Africa) kurekodi wimbo na Trey Songz.
“Katika harakati zangu za kutafuta ushindi wa Grammy katika career yangu ya muziki, inanipa nguvu kufanya kazi kwa ukaribu na Trey Songz, ambaye alishawahi kushinda tuzo hiyo,” amesema Vanessa.
Msimu mpya wa Coke Studio utaanza mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment