Friday, 7 October 2016
Vanessa Mdee aipiga chini show ya Chris Brown Mombasa
Ndoto ya Vanessa Mdee kutumbuiza kwenye jukwaa moja na msanii wa Marekani, Chris Brown kwenye tamasha la Mombasa Rocks Music Jumamosi hii imepeperuka.
Hitmaker huyo wa ‘Niroge’ ameweka wazi kupitia mtandao wake wa Instagram sababu ya kutotumbuiza kwenye tamasha hilo ni kutofikia makubaliano na waandaaji wa tamasha hilo.
Kwa sasa macho ya Vanessa yatakuwa ni kwenye tamasha la One Africa Music litakalofanyika jijini Houston, Texas, Marekani, October 22 ambapo anatarajiwa kupanda kwenye jukwaa moja na wasanii wengine kama 2 Face, Flavour, P –Square, D’Banj, Kcee, Mafikizolo, Fally Ipupa na Cabo Snoop.
Rais Magufuli ampongeza Bakhresa
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amempongeza Said Salum Bakhresa kwa kuwa mzalendo na kuongeza pato la taifa kwa kulipa kodi kupitia biashara zake.
Alisema hayo katika kijiji cha Mwandege wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani wakati akizindua kiwanda cha kusindika matunda kilichopo chini ya Kampuni ya Food Products mali ya kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) ya Dar es Salaam.
“Leo hapa kwenye kiwanda hiki cha kusindika matunda pekee, kimetoa ajira kwa Watanzania takribani 800, bado viwanda na kampuni zake nyingine zinazozalisha bidhaa kama vile maji na juisi ambazo zimetoa ajira kwa Watanzania wengi nchi nzima. Huu ndio uwekezaji ambao awamu ya tano tunauhitaji,” alisema.
Rais Magufuli pia alimpongeza Bakhresa kwa kuwa Mtanzania na mzalendo wa kwanza kuanzisha viwanda mbalimbali, ambavyo pamoja na kuchangia katika pato la taifa kwa kulipa kodi, lakini pia vinatengeneza ajira kwa watu wengi.
Said Ally, aliyetobolewa macho Buguruni Sheli hatoweza kuona tena
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa majibu
kuhusu na hatma ya kijana
Said Ally aliyetobolewa macho maeneo ya
Buguruni Sheli na kusema hatoweza kuona tena.
Makonda akimliwaza Said Ally baada ya madaktari kusema kuwa hakuna namna ya
kumfanya awe kuona tena
“Majibu yametoka na Said ameturuhusu tuyaweke wazi majibu ni mabaya ila tumeyapokea itabidi tukubaliane na matokeo kwamba ndugu yetu hataweza kuona tena kwa maisha yake yote,” alisema Makonda.
“Serikali ya mkoa imejitolea kumpatia matibabu ya macho ya bandia kwa ajili ya kutengeneza shape ya uso wake tena, kumpatia elimu ya kusoma tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira. Serikali ya mkoa imetoa gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu yake,” alisema.
Pia Makonda amesema serikali itatoa kiasi cha shilingi milioni kumi kama sehemu ya mtaji wake. “Kabla ya kupatwa na ulemavu huo, Said alikuwa kinyozi hivyo kuna mdogo wake yupo atamsaidia kwakuwa mwanzoni walikuwa wakifanya kazi pamoja,” aliongeza.
Kupitia Instagram pia, Makonda ameandika: Watanzania wengi tulitamani Said uone tena ila tumeshindwa, tuna mwachia Mungu.
Tayari mtu aliyemfanyia Ukatili huo yupo mahabusu.
New Video: Victoria Kimani – My Money
Thursday, 6 October 2016
Video: Chris Roby – Pana Cover Swahili
Video: Kid Ink – Die In It
Kid Ink transforms into a wolf in his new video for “Die in It,” which arrives just in time for Halloween.
New Video: Linah – Raha Jipe Mwenyewe
Malkia wa muziki Linah Sanga ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Raha Jipe Mwenyewe’. Ndani ya video hiyo mchekeshaji Idris Sultan amecheza vitendo. Audio imeandaliwa na producer Mr T Touch na video imeandaliwa na director, Khalfani Khalmand
VideoMPYA: DJ Khaled ametuletea hii Video yake mpya – Do You Mind
Subscribe to:
Posts (Atom)