Akiongea kwenye kipindi cha Mseto cha Radio Citizen, Jaguar alisema Chidi amekuwa akidai kuwa muziki wake hauchezwi redioni, jambo linalomchanganya na kumfanya aendelee kutumia unga.
“Chidi Benz nimeongea naye kwa muda mrefu hata nilienda TZ na kuna picha kwenye mtandao tuko naye. Kibaya kuna watu unaweza ukawasaidia na wengine usiwasaidie, mfano kama Chidi ni rafiki yangu ukiongea naye analose hope haraka sana na maisha,” alisema Jaguar.
“Kama sasa ananiambia kuna watu walikataa kucheza muziki wake, mimi tunakaa chini na AY tunaongea, tunamuambia wewe ingia studio AY atasimamia lakini unapata analose hope haraka sana. Sasa huwezi ukafanya kila kitu kwa mtu,” aliongeza
No comments:
Post a Comment