Mtoto wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja nchini India aliyebainika
kuwa na nywele kwenye sehemu zake za siri na hamu ya kufanya mapenzi
amegundulika kuwa na tatizo la homoni ambalo ni nadra sana.
Mtoto huyo ambaye jina lake ni Akash, alipatikana akiwa na homoni za
testosterone zenye kiwango cha mtu mzima mwenye miaka 25. Hiyo
inamaanisha kuwa alikuwa na uume wenye size kama ya mtu mzima, ndevu na
nywele za sehemu za siri pamoja na sauti isiyoendana na umri wake.
Madaktari sasa wanadai kuwa mtoto huyo ana tatizo liitwalo precocious puberty ambapo mtoto hubalehe kabla ya miaka saba au nane.
Wazazi wa Akash mwanzoni waligundua kuwa kuna kitu hakipo sawa kwa
mtoto wao alipokuwa na miezi sita. Uume wake ulikuwa ukiwa mkubwa kuliko
kawaida, wakati mwili wake ulikuwa mdogo mno ukilinganisha na watoto wa
umri wake.
“Tulidhani labda alikuwa mtoto mkubwa, hivyo hatukumpeleka kwa
daktari,” mama wa mtoto huyo aliliambia gazeti la Hindustan Times.
“Lakini alipofikisha mwaka mmoja, ilikuwa wazi kuwa kuna kitu hakikuwa
sawa. Mama mkwe wangu, ambaye amewalea watoto kadhaa kwenye familia pia
alisema ukuaji wake haukuwa wa asili. Hapo ndipo tulipompeleka kwa
daktari.’
Daktari wa Akash, Vaishakhi Rustagi, ameliambia Hindustan Times kuwa
tatizo hilo lina athari kwa mtoto na kwamba itafika muda atashindwa
kukua na kumfanya awe na urefu wa futi 3-4 muda wote. Mtoto huyo kwa
sasa anapewa matibabu.
Precocious puberty ni tatizo la nadra sana. msichana aliyewahi kuzaa
akiwa na umri mdogo zaidi kuwahi kutokea ni Lina Medina, aliyezaa akiwa
na umri wa miaka mitano na miezi saba huko Peru mwaka 1939, na kuwa
maarufu duniani enzi hizo.
Wazazi wake walidhani kukua kwa tumbo lake kulitokana na uvimbe
lakini baada ya tiba za mwanzo kutofanikiwa ndipo walipompeleka
hospitali.Mwezi mmoja tu baadaye aliushangaza ulimwengu baada ya
kujifungua mtoto wa kiume.
No comments:
Post a Comment