Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mh. Prof Makame Mbarawa akimpongeza Afisa Mkuu Mtendaji wa TTCL Kamugisha Kazaura baada ya kuzindua nembo mpya hivi karibuni
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema wakati umefika kwa wazee wanaofanya kazi TTCL, kuwaachia vijana.
Alisema hayo wakati akizindua nembo mpya ya kampuni hiyo na mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE wiki iliyopita. Profesa Mbarawa alisema wazee wamekuwa watu wa kuzungumza zaidi ofisini, kuliko kufanya kazi na kubuni mbinu mpya zenye kuhimili ushindani.
Alisema uzinduzi wa nembo mpya katika kampuni hiyo, hautakuwa na maana ikiwa wafanyakazi wa kampuni hiyo hawatabadilika na kutoa huduma zitakazowavutia wateja. Aliishauri menejimenti kutoajiri watumishi kwa kujuana, bali watoe fursa kwa vijana wenye uwezo wa kuhimili ushindani unaotokana na mabadiliko ya teknolojia ya mawasilian
No comments:
Post a Comment