Kila siku asubuhi huwa nazisogeza
headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi
wa stori zote napandisha kwenye hsabai.com Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa
chini moja baada ya nyingine.
Stori kubwa kwenye magazeti ya leo June
09 2016 ni kuhusu Bajeti ya mwaka 2016/2017, moja ya stori iliyochomoza
ni hii kwenye gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Mikoa mitano maskini zaidi Tanzania hii hapa”
Serikali imesema kuwa Kigoma, Geita, Kagera, Singida na Mwanza ndiyo mikoa mitano maskini zaidi nchini, aidha mikoa ya Dar es salaam, Kilimajaro, Arusha, Pwani na Manyara ndiyo mikoa mitano yenye ahueni ya umaskini nchini
Waziri wa fedha na mipango Dk Phillip
Mpango alisema hayo jana wakati akiwasilisha bungeni taarifa ya hali ya
uchumi ya mwaka 2015 na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa fedha
2016/17.
Waziri Mpango alisema tathmini ya hali
ya umaskini kimaeneo iliyofanyika kwa kutumia takwimu za sensa ya watu
ya mwaka 2012 na utafiti wa hali ya kipato na matumizi katika kaya wa
mwaka 2012,unaonyesha matokeo chanya na kutofautiana kimkoa na wilaya
Waziri Mpango alisema mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kuwa na umaskini mkubwa wa 48.9% ukifuatiwa na Geita (43.7%), Kagera (39.3%), Singida (38.2%) na Mwanza (35.3%).
No comments:
Post a Comment