June 22
2016 Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amehutubia katika Jubilei ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT)
iliyofanyika katika ukumbi wa Benki hiyo, mtaa wa Mirambo Jijini Dar es
salaam.
Katika
hotuba yake Rais Magufuli amesema serikali imeamua kusimamisha kwa muda
mfupi usiozidi miezi miwili zoezi la utoaji ajira mpya na upandishaji
wa vyeo kwa watumishi wa umma kwa lengo la kupisha uhakiki wa watumishi
wa umma katika orodha ya malipo ya mshahara na kuondoa watumishi hewa.
Rais Magufuli
amesema zoezi hilo halina nia ya kuwakatisha tamaa watumishi wa umma na
amewahakikishia watumishi wote wa umma kuwa serikali itaendelea kuajiri
watumishi wapya na kuwapandisha vyeo waliopo kama kawaida mara baada ya
kukamilika kwa zoezi, Rais Magufuli amesema……….
>>>’Serikali
ninayoiongoza haina nia ya kuwakatisha tamaa wafanyakazi, lengo lake ni
kujipanga kwa makosa tuliyoyafanya, na ndio maana nimesema kwa kipindi
cha mwezi mmoja hivi au hata mwezi mmoja na nusu, haitazidi miezi
miwili, tusiajiri mtumishi yeyote serikalini’
>>>’katika
kipindi cha mwezi mmoja hatutawapandisha vyeo wafanyakazi, ninaomba
wafanyakazi waelewe hili, kwa sababu tukiendelea tutakuwa tunawapandisha
vyeo hata wafanyakazi ambao hawapo, tunafanya ukaguzi wote
tukishamaliza wafanyakazi wataendelea kupandishwa vyeo” amesema Rais
Magufuli’:-Rais Magufuli
ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI ALIVYOKWENDA BENKI KUU BILA KUWATAARIFU ? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment