Moja ya stori iliyoripotiwa ni hii kwenye gazeti la Habari Leo yenye kichwa cha habari ‘Mabasi ya haraka kuanza kutumia gesi’
Gazeti la
Habari Leo limeripoti kuwa` msimamizi wa usambazaji gesi katika shirika
la maendeleo ya petrol Tanzania (TPDC), Ismail Naleja, amesema awamu ya
pili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam yatatumia nishati
ya gesi asilia badala ya mafuta jambo litakalosaidia kupunguza gharama.
Kupitia gazeti hilo Naleja amesema
matumizi ya nishati hiyo yataanza katika awamu ya pili ambapo mabasi
mapya 200 ya mradi huo yanatarajiwa kuingizwa nchini.
Akizungumza
katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam
yanayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu Nyerere, kuhusu usambazwaji wa
gesi katika magari, Naleja alisema hatua hiyo itaongezeka idadi ya
magari yanayotumia gesi nchini ambapo hivi sasa kuna mabasi 60
yanayotumia gesi na kuwashauri wenye magari kutumia mfumo huo ili
kupunguza gharama za uendeshaji.
>>>’‘Uendeshaji
wa gesi utakua nafuu jambo linaloweza kufanya hata nauli zake kupungua
kwani kilo moja ya gesi itatumika katika umbali unaotumiwa na mafuta ya
dizeli lita moja na nusu”
No comments:
Post a Comment