Ya kufahamu baada ya mkutano na Benki ya Dunia Ikulu kuhusu Fly Over Ubungo
Waziri wa Fedha Tanzania Dr. Philiph Mpango amewaeleza Watanzania kila kilichosemwa kwenye mazungumzo IKULU na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ambaye ameitembelea Tanzania ambapo moja ya vilivyojadiliwa ni Fly Over ya Ubungo ambayo itasaidia sana kuondoa foleni sugu.
- Kulikua na mazungumzo rasmi
yaliyofanyika IKULU na kubwa la kwanza ilikua ni kuihakikishia benki ya
Dunia kwamba kwa kweli ni wabia wetu wazuri wa maendeleo na Rais
amesisitiza kwa upande wa serikali tutaendelea kufanya kazi kwa ukaribu
na benki ya dunia.
- Eneo moja ambalo Rais ameiomba
Benki ya dunia itusaidie kuharakisha kuanza utekelezaji ni pale Ubungo
kwenye makutano ya zile barabara.
- Huu mradi wa Mabasi yaendayo
kazi hautakuwa na ufanisi kama bado pale Ubungo utategemea Askari wa
barabarani kuongoza magari kwahiyo Rais Magufuli amesisitiza zaidi.
- Makamu wa Rais wa Benki ya
Dunia amekubali kwamba wataharakisha ule mchakato ili ujenzi wa barabara
za juu kwenye makutano ya barabara Ubungo uanze.
- Kuhusu gharama za ujenzi wa
Fly Over Ubungo hatuna namba kamili kwa sasa kwasababu bado
tunakamilisha majadiliano lakini kwa takwimu za awali haitapungua Dola
za Kimarekani MILIONI 60
No comments:
Post a Comment