Thursday, 6 October 2016
VideoMPYA: Shilole anatukaribisha kuitazama hii video yake mpya
Monday, 3 October 2016
VideoMPYA : Baraka Da Prince na Alikiba wametuletea video yao mpya
Ni Single mpya iitwayo Nisamehe ambayo ilirekodiwa April 27, 2016 kwenye studio za producer Emma The Boy na wakali kutoka kwenye label ya Rockstar 4000 Baraka Da Prince na Alikiba
Sasa leo kupitia kwenye ukurasa
wa instagram wa Alikiba aliwasuprise mashabiki wao baada ya kuachia
video mpya ya single hiyo iitwayo Nisamehe.
Ukishamaliza kuitazama hii video sio mbaya ukituachia na comment yako wakali hawa watapita hapa kujua Watanzania wameipokeaje.
New Video: Davido – Gbagbe Oshi
Davido ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Gbagbe Oshi’ ambao utapatikana kwenye albamu yake ya ‘Son of Mercy’ iliyoanza kupatikana kama Ijumaa iliyopita. Tazama hapa chini video hiyo.
Alikiba na Vanessa Mdee kutumbuiza na Chris Brown Mombasa
.

Alikiba na Vanessa Mdee watapanda jukwaa moja na nyota wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown
Wawili hao watatumbuiza pamoja na Chris Brown, Oktoba 8, mwaka huu kwenye tamasha la Mombasa Rocks Music.
“Mombasaaaaaa it’s ME N U this weekend. @mombasarocksfestival


#Juu #Niroge,” ameandika Vanessa kwenye Instagram.
Nyota wa Nigeria, Wizkid naye atatumbuiza kwenye tamasha hilo kubwa.
Alikiba na Vanessa Mdee watapanda jukwaa moja na nyota wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown
Wawili hao watatumbuiza pamoja na Chris Brown, Oktoba 8, mwaka huu kwenye tamasha la Mombasa Rocks Music.
“Mombasaaaaaa it’s ME N U this weekend. @mombasarocksfestival
Nyota wa Nigeria, Wizkid naye atatumbuiza kwenye tamasha hilo kubwa.
Sunday, 2 October 2016
Simba na Yanga zapigwa marufuku na serikali kuutumia uwanja wa Taifa
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ametembelea Uwanja taifa Jumapili hii na kuzipiga marufuku mechi zote za Yanga na Simba kufanyikia uwanjani hapo kutokana na uharibifu wa mageti na viti uliojitokeza siku ya jana katika mechi hiyo ya watani hao wa jadi.
Mashabiki wa Simba wakitawanywa kwa mabomu ya machozi hapo jana baada ya kufanya uharibufu wa viti
Pia Nape amezuia mapato ya timu hizo ya mchezo wa jana kutokana na uharibifu huo.
“Simba na Yanga hawatoutumia tena uwanja huu mpaka pale Serikali itakapoona kuwa mazingira yanaruhusu,” alisema Nape. alisema Nape.
Amri hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya mashabiki wa klabu ya Simba, kung’oa viti vilivyopo kwenye majukwaa ya uwanja huo kwa kile walichokidai kupinga uamuzi wa Refa, Martin Saanya aliyechezesha mechi hiyo. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Tazama kionjo cha video ya ‘Nisamehe’ ya Barakah The Prince na Alikiba
Video ya wimbo wa Barakah The Prince aliomshirikisha Alikiba, Nisamehe itaanza kuoneshwa kwa mara ya kwanza, Jumanne, Oktoba 4 kupitia MTV Base. Video hiyo ilifanyika Afrika Kusini na kuongozwa na Meji Alabi. Chini ni kionjo chake.
Video: Bondia afariki dunia baada ya kupokea kichapo ulingoni
Bondia Mike Towell (25) amefariki dunia baada ya kupoteza pambano lake na Dale Evans kwenye mzunguko wa tano. Pambano hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa St Andrews Sporting Club Alhamisi iliyopita. Baada ya kupoteza pambano hilo hali yake ilibadilika na kukimbizwa hospitali ambako baadaye alifariki dunia. Ripoti ya madaktari imeonesha kifo cha Mike kimesababishwa na kuvujiwa na damu nyingi kwenye ubongo baada ya fuvu lake kupata madhara. Kabla ya kupoteza pambano hilo bondia huyo aliangushwa mara mbili kwenye mzunguko wa kwanza kabla ya kuangushwa tena kwa konde zito na kushindwa kuendelea na pambano.
Video: Diamond abaki na nguo ya ndani ‘boxer’ wakati akisherekea birthday yake
Jumamosi hii ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya staa wa muziki, Diamond Platnumz ikiwa ni wiki moja toka atoke visiwani Zanzibar kusherekea birthday ya mama watoto wake, Zari.
Muimbaji huyo alikata keki mbele ya wasanii wake wa WCB huku akiwaacha midomo wazi mashabiki wake wa kwenye mitandao jamii kwa kitendo cha kusherekea birthday hiyo huku akiwa na nguo ya ndani ‘boxer’ akidai alikuwa anaogopa kumwagiwa maji. Pia mastaa mbalimbali walimtumia salamu za heri na baraka staa huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Salome’. Rich Mavoko Happy Birthday Big Nna Zawadi Yako Ya Gari Lakini La Udongo 😂😂 So Wambie Hao Wanaokumwagia Maji Nikilileta Waache Kwanza Harmonize Happy birthday my brother #simbaa nikisema niandike mengi sitomaliza ila unajuwa vyenye nakuzimia na na kukuheshimu….🙏🙏🙏 maisha marefu furahiya siku yako 🎂🔥🔥 Rayvanny Jus me and birthday boy @diamondplatnumz Bigie Mungu Akupe Maisha Marefu ndugu yangu maana ukinasa hatunasuliki mwiiiiiiiiingiiiiiiiii wa materials enjoy your day
Friday, 30 September 2016
PICHA: Majiji yanayoongoza kwa kutembelewa zaidi duniani
Leo September 26, 2016 nafahamu utakua unayajua majiji mengi kutoka kwenye nchi tofauti
tofauti na huenda umeshatembelea huko au kwa kuyaona kwenye picha, Sasa
leo nakusogezea hapa list ya Majiji yaliyotajwa na taasisi ya The Mastercard’s Global Destination Cities Index ikiyaweka kwenye majiji yanayotembelewa zaidi duniani.
List hii
imetoka baada ya kukusanya taarifa za majiji hayo za miaka Saba kuanzia
mwaka 2009 mpaka 2016. Bara la Asia limechukua headlines kwa kuingiza
Majiji 11, wakati hakuna jiji lolote lililoingia kutoka Bara la Afrika.
Hii ndio List kamili ya majiji 20 yaliyotajwa kutembelewa zaidi duniani.
20. Prague, Jamhuri ya Czech
Jiji hili limetajwa katika nafasi ya 20 likiwa idadi ya watu Milioni 5.81 wanaolitembelea kika siku.
19. Shanghai, China
Hutembelewa na watu Milioni 6.12 kwa siku.
18. Vienna, Austria
Hutembelewa na watu Milioni 6.69 kila siku.
17. Osaka, Japan
Hutembelewa na watu Milioni 7.02 kila siku.
16. Roma, Italy
15. Taipei, Taiwan
Hutembelewa na watu Milioni 7.35 kila siku.
14. Milan, Italy
Hutembelewa na watu Milioni 7.65 kila siku.
13. Amsterdam, Uholanzi
Hutembelewa na watu Milioni 8 kila siku.
12. Barcelona, Hispania
Hutembelewa na watu Milioni 8.2 kila siku.
11. Hong Kong, China
Hutembelewa na watu Milioni 8.37 kila siku.
10. Seoul, Korea Kusini
Hutembelewa na watu Milioni 10.2 kila siku.
9. Tokyo, Japan
Hutembelewa na watu Milioni 11. 7 kwa siku.
8. Istanbul, Uturuki
Hutembelewa na watu Milioni 11.95 kila siku.
7. Kualar Lumpur, Malaysia
Hutembelewa na watu Milioni 12.02 kila siku.
6. Singapore
Hutembelewa na watu Milioni 12.11 kila siku.
5. New York, Marekani
Hutembelewa na watu Milioni 12.75 kila siku.
4. Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu
Hutembelewa na watu Milioni 15. 27 kila siku.
3. Paris, Ufaransa
Hutembelewa na watu Milioni 18.03 kila siku.
2. London, Uingereza
Hutembelewa na watu Milioni 19.88 kila siku.
1. Bangkok, Thailand
Hutembelewa na watu Milioni 21.47 kila siku.
RIPOTI ya Benki ya Dunia kuhusu Uchumi wa Tanzania na Rwanda iko hapa..
Taarifa hii kutoka Benki ya Dunia ambayo imetoa ripoti
ya ustawi wa uchumi wa Afrika ambapo nchi za Afrika Mashariki za
Tanzania na Rwanda zinaonekana kuwa na uchumi wenye kustawi kwa wastani.
Ripoti
mpya ya Benki ya dunia itolewayo mara mbili kwa mwaka, Africa’s Pulse,
inaonesha kuwa mwelekeo wa ukuaji uchumi barani Afrika unatarajiwa
kudorora zaidi na kuwa asilimia moja nukta sita mwaka huu ikilinganishwa
na asilimia tatu mwaka jana.
Hata hivyo
imebainisha kuwa, mwelekeo wa ukuaji unatofautiana ambapo baadhi ya
nchi ustawi umedorora huku nyingine uchumi unakua. Kwa mfano Rwanda,
Tanzania na Ethiopia zimetajwa kuwa nchi zenye ustawi wa wastani ambao
ni zaidi ya asilimia sita kwa mwaka, huku Cote d’Ivoire na Senegal
zikiongoza kwa kasi ya ustawi barani Afrika.
Mchumi
Mkuu wa Benki ya dunia kuhusu Afrika Albert Zeufack amesema chanzo cha
kukwama ustawi wa uchumi ni kudorora kwa bei za bidhaa ikiwemo mafuta,
hali ngumu ya kifedha na sera za uchumi zisizo makini.
Benki ya
Dunia inasema mwelekeo ni kupanua wigo wa bidhaa zinazouzwa pamoja na
kuboresha sekta ya kilimo hasa kwa wakulima wadogo wadogo ili kuinua
vipato vyao na kupunguza umaskini.
Subscribe to:
Posts (Atom)