HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Wednesday, 25 January 2017

Nchi 7 ambazo raia wake watazuiliwa kuingia Marekani maneno ya Trump



Taarifa za baadhi ya maafisa wa bunge la Marekani (Congress) na mtaalamu katika Idara ya Uhamiaji zimeeleza kwamba Rais Trump leo Jumatano anatarajia kusaini miswada kadhaa ikiwemo ya kusimamisha kwa muda utoaji visa kwa raia wa nchi za Kiarabu.
January 25, 2017 Trump aliandika kwenye Twitter kwamba itakuwa siku kubwa kwa usalama wa taifa, pamoja na mambo mengine tutajenga ukuta.
Ufafanuzi uliotolewa umeeleza kuwa Trump anakusudia kuzuia kwa miezi kadhaa wahamiaji kuingia Marekani isipokuwa wale aliowataja kuwa ni wa “Jamii za wachache wanaodhulumiwa” hadi zitapopitishwa sheria kali na ngumu kuhusiana na uingiaji wakimbizi nchini humo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, maombi ya vibali kwa raia wa Syria, Iraq, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen vitazuiliwa.
Vilevile katika ukurasa wake Twitter, Trump ameonesha pia msimamo wake wa kujenga ukuta kwenye mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Mexico na kusisitiza kuwa ujenzi huo utatekelezwa kwa namna yoyote.

Rayvanny azungumzia mpango wa kuachia wimbo mpya



Msanii wa muziki kutoka WCB, Rayvanny amedai ataachia wimbo wake mpya muda mchache baada ya kutoka kwa video ya wimbo ‘Kijuso’ alioshirikishwa na Queen Darlin.

Muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na wimbo ‘Natafuta Kiki’ amedai ameandaa kazi nyingi ambazo zinasubiri wakati wa kutoka.
Akizungumza na mashabiki wake live katika mtandao wa Instagram (Insta Live) Jumanne hii, Rayvanny amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya ujio wa kazi mpya.
“Mashabiki wangu soon nitaachia wimbo mpya, sema itaanza kwanza kutoka video ya ‘Kijuso’ na baada ya hapo ndo mzigo unaweza kutoka,” alisema Rayvanny.
Muimbaji huyo toka aachie wimbo ‘Natafuta Kiki’, ameshirikishwa kwenye ngoma zaidi ya 3 ambazo ni pamoja Salome aliyoshirikishwa na Diamond, Kijuso na Queen Darlin pamoja na Mugacherere na Q Boy.

Tuesday, 24 January 2017

NEW SECRET DESIGN RANGE ROVER DISCOVERY ADVANCE 2017

Baby Madaha Amkimbia Chidi Benzi Stendi Alipokuwa Akipiga Debe

Kampuni ya Nokia yaweka rekodi ya kuuza simu zake mpya ‘Nokia 6’ ndani ya dakika 1


Kampuni ya Nokia imerudi upya katika ulimwengu wa ushindani wa simu za Smartphone zenye mfumo wa android baada ya wiki hii kuingiza sokoni simu mpya aina ya Nokia 6 na kuuzika kwa muda wa dakika moja.

Nokia kwa sasa ipo chini ya kampuni ya HDM Global na liliuza simu za Nokia 6 huko nchini china tuu na ndipo walipopata matunda makubwa.
Mauzo ya simu hii yalifanyika katika mall ya JingDong, na watu ambao walijiandikisha mwanzoni kabisa kabla hata ya simu haijafika hapo ili ikifika wawe wakwanza kuipata walikua ni zaidi ya milioni moja na laki tatu.
Japokuwa haijulikani kwa undani kuwa Nokia iliuza simu ngapi ndani ya dakika hiyo moja lakini kinachojulikana ni kwamba ziliisha zote ambazo zilikuwa katika stoo.

Nokia ilikua inauzika china kwa gharama ya yuan 1699 ambayo ni ni sawa na dola 248 za kimarekani na kwa haraka haraka ni sawa na laki tano za Tanzania.
Pengine sifa za simu hii ndio zimeipa umaarufu mkubwa ukiachana na kuwa kampuni ya Nokia kwa kipindi cha muda mrefu imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa inatengeneza simu ambazo ni imara na zinazodumu kwa muda mrefu.

Joti aeleza kwanini Orijino Komedi haipo kwenye TV siku hizi

Kwako mfatiliaji wa mabingwa wa kuchekesha wanaoishikilia rekodi ya Wachekeshaji waliotazamwa sana kwenye TV Tanzania kuanzia time hiyo ya ZE Comedy mpaka Orijino Komedi walivyokua wanawafanya watu wawahi TV zao kila Alhamisi jioni.
Ni kitambo kidogo hatujawaona Orijino Komedi kwenye TV (TBC 1) na inawezekana maswali tuliyonayo ni mengi lakini hakuna hofu tena maana tumempata Joti na amekubali kuongelea kwa ufupi.
Kama kundi tunataratibu zetu na ndio maana tumejaribu kutumia muda wa mwaka mmoja kupumzika maana toka tuanze kufanya kazi hatujawahi kupumzika, tulivyopomzika pia sio kukaa kimya tukaangalia project za kila mtu binafsi na ndio maana unaona kila mtu na shughuli zake‘ – Joti
Ukimfatilia Mpoki kuna shughuli zake anafanya na inajulikana, Masanja pia vivyo hivyo… na mimi nimefungua Youtube channel yangu ya Joti TV, nafikiri mwaka huu tunaweza kurudi kazini pia‘ – Joti

Je wajua nini hufanya macho yaonekane mekundu ukipiga picha kwa kutumia kamera yenye flash?

Macho hutupa uwezo wa kuona vitu vinavyotuzunguka zaidi ya vile ambavyo panya na viumbe wengine wanavyoona na kujenga uwezo wao wa kufikiri.


Mwanga huingia ndani ya jicho kupitia cornea. Baada ya hapo mwanga hufanyiwa utambuzi na retina na taswira hupelekwa moja kwa moja kwenye ubongo kupitia optic nerve. Kiasi cha mwanga kinachoingia kwenye retina hudhibitiwa na pupil. Wakati wa mchana sababu kuna mwanga mkali, pupil husinyaa na kuruhusu mwanga kidogo kuingia ndani ya jicho.
Wakati wa giza, pupil hutanuka kuruhusu mwanga wa kutosha kuingia. Katikati ya retina na sclera (sehemu nyeupe ya jicho) kuna kiwambo chenye tishu zinazoitwa Choroid. Safu hii husambaza damu, virutubisho na oksijeni katika maeneno ya nje ya retina. Choroid ina mishipa mingi sana ya fahamu.
Mwanga wa flash ya camera unapotoka, pupil huwa haipati muda wa kutosha kusinyaa, hivyo basi kiasi kikubwa cha mwanga huakisiwa (reflected) na fundus (sehemu ya mbele ya jicho). Kutokana na choroid kuwa na mishipa mingi ya damu, hivyo basi mwanga unaochukuliwa na lensi ya kamera huonekana mwekundu. Mtu akiangalia picha yake ataona macho yake yanaonekana mekundu.
Kutokana na angle ambayo mwanga huingia kwenye jicho ni sawa na engo (angle) ambayo mwanga huakisiwa kutoka nje, na jinsi flash inavyokuwa karibu na lensi ya kamera ndivyo kunavyokuwa na uwezekano mkubwa wa mwanga ulioakisiwa kuonekana na lensi.
Sababu nyingine inawezekana kuwa ni kiasi cha melanin kwenye kiwambo nyuma ya retina na umri wa mtu anayepigwa picha. Watu weupe (light skinned people) wenye macho yenye rangi ya blue huwa wanakuwa na kiasi kidogo cha melanin kwenye fundus zao hivyo basi uwezekano wa macho yao kuonekana mekundu ni mkubwa kuliko watu weusi (dark skinned people) ambao wengi wao huwa na macho yenye rangi ya kahawia (brown).
Watoto wadogo pia wakipiga picha na kamera yenye flash kuna uwezekano mkubwa kwenye picha akaoneka ana macho mekundu, hii inatokana na ukweli kuwa pupils za macho ya watoto hutanuka kwa haraka kuliko za wakubwa

PICHA : Kwa mwaka hii ndio miji ya gharama zaidi kuishi dunian 2017


Wakati watu mbalimbali  Tanzania wakilalamika hela imepotea, leo nimekutana na miji ambayo ni gharama zaidi kuishi mwaka 2017 Duniani kutokana na soko la Nyumba kuwa juu zaidi duniani.
1. Hong Kong, China
2. Sydney, Australia
3. Vancouver,  Canada
4. Auckland, New Zealand
5. San Jose, Marekani
6. Melbourne, Australia
7. Honolulu, US
8. Los Angeles, Marekani
9. San Francisco, Marekani
10. Bournemouth & Dorset, Uingereza