HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Wednesday, 21 September 2016

Video: Rick Ross – Same Hoes

What does a Rick Ross pool party look like? Rozay invites fans to an epic backyard bash in his latest video for “Same Hoes.”

Tuesday, 20 September 2016

VIDEO: Ndege mpya ya Air Tanzania ilivyowasili Dar leo

Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.
Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake (Water Salute).
Baada ya kupokewa ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga). Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye.

Sunday, 18 September 2016

VIDEO: TOP 10 ya nyumba za gharama zinazomilikiwa na mastaa wa Basketball



Rekodi za mastaa wa michezo kumiliki vitu vya thamani kubwa sana yakiwemo magari expensive, biashara za mavazi na hasa viatu na nguo zimekua zikiwekwa kila wakati. Wapo mastaa wapya na wakongwe kama Michael Jordan ni mmoja kati ya mastaa waliofanikiwa kuingia kwenye headlines za kuwa na mkwanja mrefu baada ya kuendelea kushikilia deal yake na kampuni ya Nike ambao ni watengenezaji wa viatu vya Air Jordan au J 23.
Leo nakuletea list ya nyumba kumi kali sana za mastaa wa mpira wa kikapu duniani.

VideoMPYA: Diamond Platnumz na Rayvanny wanatualika kuitazama hii ‘Salome’

Wakali kutokea kiwanda cha Bongofleva Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz pamoja na Raymond a.k.a Rayvanny wakitokea katika Laber ya WCB leo September 18 2016 wanayofuraha kushare na sisi mdundo wao mpya unaoitwa ‘Salome‘ 
Tayari nimekusogezea hapa chini video yao, ukimaliza kuitazama niachie comment yako kuniambia wametisha kwa asilimia ngapi.

Kurekodi na Trey Songz ni mwanzo wa kutimiza ndoto yangu ya kushinda Grammy – Vanessa Mdee




vanessa-8

Na sasa anaamini kuwa, mwanzo wa kukaribia kuiishi ndoto hiyo umewadia. Vee Money, ni mmoja wa wasanii wa Afrika, waliochaguliwa kurekodi wimbo na mshindi wa Grammy na nyota wa RnB nchini Marekani, Trey Songz. Shukrani kwa kipindi cha Coke Studio Africa (International Week) msimu wa 4, kinachomdondosha staa huyo.
Akiwa pia anawania tuzo ya Loeries za Afrika Kusini kwa kazi yake ya video bora, Niroge, Vanessa anaungana na Rema Namakula (Uganda), Yemi Alade (Nigeria), Neyma (Mozambique), Serge Beynaud (French West Africa), Lij Michael (Ethiopia), Stonebwoy (Ghana), Nyashinski (Kenya) na Emtee (South Africa) kurekodi wimbo na Trey Songz.
“Katika harakati zangu za kutafuta ushindi wa Grammy katika career yangu ya muziki, inanipa nguvu kufanya kazi kwa ukaribu na Trey Songz, ambaye alishawahi kushinda tuzo hiyo,” amesema Vanessa.
Msimu mpya wa Coke Studio utaanza mwezi ujao.

Diamond kumsaini msanii wa nje ya Tanzania, WCB



Diamond Platnumz amethibitisha kuwa kwa yupo kwenye mipango ya kuongeza nguvu kwenye lebo yake ya WCB kwa kumsaini msanii wa nje ya Tanzania
.
14063607_1600205776943920_1390840306_n
Hitmaker huyo wa Kidogo amesema hayo wakati akijibu swali la shabiki kwenye mtandao wa Twitter, lililokuwa linauliza “WCB hamjafikiria kusaini msanii nje ya Tanzania au mtafanya?”
Diamond alijibu swali hilo kwa kuandika, “Soon.”
diamond-1
diamond
Aidha muimbaji huyo amesema kuwa kolabo za wasanii wake wa WCB ambazo wamefanya na wasanii wa nje zipo tayari.

Video: Ado Tembo ft Peter Msechu – Okoa Mtoto

Tukitaka kufanya Tanzania na Afrika kuwa mahali salama kuishi ni lazima tuanze na mtoto, nikiwa na maana tukimpenda mtoto,tukimlinda,tukimjali na kumthamini mtoto bila shaka tutakuwa tumefanya Africa kuwa mahala rafiki pa kuishi kwani mtoto ni Rais wa kesho,Waziri wa kesho,Mbunge wa kesho,Dakatari wa kesho,Mwalimu wa kesho,Ni mwanamuziki wa kesho n.k Inaanza na mimi,Inaanza na wewe,Inaanza na yule.

Saturday, 17 September 2016

Video: P Square wameileta hii mpya inaitwa ‘Bank alert’

Kutoka Lagos Nigeria, Afrika… kutana na mpya kutoka kwa P Square inaitwa ‘bank alert‘ na inakua video nyingine wao kuonekana pamoja baada ya ile ya Diamond toka stori za wawili hawa kugombana ziliposambaa.

Behind the scenes: Video ya RayVanny ‘Natafuta kiki’


Video hiyo mpya ilitayarishwa na KWETU STUDIO

Video: Alice kella – Siri Si Siri

Msanii mwenye sauti ya kipekee katika mziki wa bongo fleva Alice kella ameachia video mpya ya wimbo “Siri Si Siri”, Video imeongozwa na Jukya kutoka Goba Studios.